Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, July 11, 2011

Wabunge Wasifu Uwezo Wa Kampuni ya IRIS, Iliyoshinda Zabuni Ya Kutengeza Vitambulisho Vya Kitaifa


Mheshimiwa Anna Abdalah,Kiongozi wa msafara wa Kamati Maalumu ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,iliyopewa jukumu la kwenda nchini Malaysia,kuchunguza na kubaini uwezo wa Kampuni ya IRIS ya nchini humo,ili kubaini uwezo wa kampuni hiyo kutekeleza jukumu muhimu la kutengeneza vitambulisho vya Kitaifa. Mheshimiwa Anna Abdala,alisema kuwa watanzania hawana sababu ya kuhofia uwezo wa kampuni hiyo kwani ni kampuni kubwa na ina wataamu na teknolojia ya hali ya juu ya kutengeza vitambulisho ambavyo ni vigumu mno kughushiwa na havichakai haraka.Alisema kuwa Kampuni ya IRIS imetengeza Vitambulisho vya Utaifa kwa nchi mbali mbali Duniani.
Mbunge wa Maswa,John Shibuda,akizungumza na waandishi wa habari jana mchana,Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuwasili kutoka nchini Malaysia ambako yeye na wabunge wenzake walikwenda kuchunguza sambamba na kubaini uwezo wa kampuni ya IRIS ya nchini humo iliyopewa zabuni ya kutengeza vitambulisho vya Kitaifa.Shibuda aliishauri serikali kutenga bajeti haraka kwa ajili ya kuanza mradi wa kutengeneza vitambulisho vya Kitaifa.Aliongeza kusema kuwa umuhimu wa Watanzania kuwa na Vitambulisho vya Kitaifa haukwepeki.
Waheshiwa wabunge wakipata chai Jana asubuhi,mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,Dar es Salaam,wakitokea nchini Malaysia,ambako walikwenda kuchunguza sambamba na kubaini uwezo wa kampuni IRIS,iliyoshinda na kupewa zabuni ya kutengeneza vitambulisho vya Kitaifa.
Baadhi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.Picha na Victor Makinda
Habari kwa hisani ya Haki Ngowi



No comments: