Baadhi ya wakazi wa mjini Iringa wakiwa ndani ya uwanja wa Samora,jioni ya leo kushuhudia tamasha la Serengeti Fiesta 2011,ambapo tamasha hilo liliwakutanisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya.
Msanii wa kike aitwaye Dayana akiimba jukwaani jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011.
| Msanii wa muziki wa kizazi kipya Top C akiimba jukwaani. |
Msanii wa muziki wa kizazi kipya na Prodyuza wa studio ya Sharobaro Records,Bob Jr a.k.a Rais wa Masharobaro pichani kulia akiimba jukwaani sambamba na madensa wake,mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Iringa (hawapo pichani) waliojitokeza jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011.
Baaabu kutoka Gangwe Mob,Inspekta Haroun akiwarusha wakazi wa Iringa jioni ya leo.
Msanii wa Bongofleva Jaffarai akiwaimbisha mashabiki wake jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011.
Mkali mwingine wa miondoko ya Hip Hop Izzo Bizzness akishusha mistari.
Anaitwa Godzilla kutoka Sala sala jijini Dar, ni mmoja wa wasanii wa hip hop wanaondelea kuzikonga nyoyo za mashabiki wake kwa namba ambayo anashusha mistari bomba kabisa awapo jukwaani.
Mwana-FA nae hakuwa nyuma kuwakuna wakaiz wa Iringa jioni ya leo kwenye tamasha la msimu wa dhahabu na serengeti fiesta 2011.
Watu walikuwa kibao ndani ya uwanja wa samora jioni ya leo.
Mkongwe wa muziki kizazi kipya,Prof Jay akiwakumbushia baadhi ya nyimbo zake,mashabiki waliokuwa wamefika kwenye tamasha la msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta 2011,ndani ya uwanja wa Samora,mjini Iringa.
20% kama kawa
Msanii mwinguine anaekuja juu katika anga ya muziki wa hip hop aitwaye Roma akiwaimbisha wakazi wa Iringa jioni ya leo.
Habari kwa Hisani ya Jiachie Blog

















No comments:
Post a Comment