Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, July 23, 2011

RAIS KIKWETE MGANI RASMI SIKU YA MASHUJAA

NA JOSEPH ISHENGOMA
MAELEZO, MTWARA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete keshokutwa (25/07/2011) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kumbukumbu ya Mashujaa itaayofanyika kitaifa Naliendele, Mtwara.


Kwa mujibu wa ratiba ya Maadhimisho iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Rais akiwa katika uwanja wa kumbukumbu ya mashujaa wa Naliendele, atawaongoza viongozi wenzake kuweka silaha za asili katika mnara wa mashujaa.

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Rais ataweka Mkuki na ngao, wakati Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama ataweka sime. Kiongozi wa Mabalozi nchini ataweka shada la maua, Meya wa Manispaa ya Mtwara- Mikindani ataweka upinde na mishale na Mwenyekiti wa Tanzania Legion ataweka shoka.

Baada ya tukio hilo, kutakuwepo na sala kutoka kwa viongozi wa dini akiwemo Sheikh kwa niaba ya Waislam, Mchungaji kwa niaba ya C.C.T na Padre kwa niaba ya Roman Cathoric.

Aidha gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama litatoa heshima kwa Mhe. Rais na kupiga wimbo wa Taifa kabla ya Rais Kikwete kutembelea makaburi na nyumba ya makumbusho ya Naliendele.


Sherehe hizo zinazotarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

No comments: