Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, July 14, 2011

MIAKA 50 YA UHURU WANANCHI LUDEWA HAWAJAONA LAMI

Mtoto wa kijiji cha Mndindi Ludewa akitoka shamba
Ludewa bado madaraja ni ya mbao pamoja kama inavyoonekana pichani
Watoto wa Kijiji cha Mndindi Ludewa wakitoka kusaka kuni
UBOVU wa miundo mbinu ni chazo cha umaskini kwa wakazi wa kata ya Mavanga ,Mundindi na Ibumi ambazo ni miongoni mwa kata za pembezoni mwa wilaya ya Ludewa mkoani Iringa na Tanzania ambayo pia zinaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula.
Tanzania ipo mbioni kusherehekea miaka 50 ya uhuru wake Desemba 9mwaka huu huku wananchi walio wengi ambao wanashi pembezoni mwa miji wakiwa bado mateka wa umasikini wa kipato na kujikuta wakisubiri maisha bora pasipo matumaini .
Umasikini unaoendelea kuwakumba wakazi wa pembezoni mwa miji hasa katika wilayani Ludewa unatoa picha halisi ya wilaya nyingine za Tanzania ambazo pia zitaungana na watanzania wa vijijini kuadhimisha miaka 0 ya uhuru kwa kilio cha umasikini wa kipato umasikini ambao umechangia kwa kiasi wanawake na walemavu kuendelea kunyanyasika zaidi katika familia zao
Pamoja na kuwa Tanzania ipo katika harakati za kuadhimsha miaka 50 ya Uhuru wake ila bado maisha ya wananchi wa kata hizi mbili bado ni ya kubahatisha na kujikuta wakiwa katika harakati za kujikomboa kutoka katika dimbwi la umasikini.
Kata ya Mundishi ni kati ya kata 25 zilizopo Wilayani Ludewa na . Kata hii kijiografia inapakana na kata ya Mavanga na Mkoa wa Ruvuma upande wa mashariki, kata ya Madili, Lugarawa na Ludende upande wa magharibi Wilaya ya Njombe upande wa kaskazini na kata ya Ibumi upande wa kusini .na ni kata inayoundwa na vijiji vitatu Muhindi, Amani na Njelela. Kata yenye jumla ya wakazi 8412 ikiwa ni wanawake 4460 na wanaume 3952.
Wakati kata ya Kata ya Ibumi inapakana na kata ya Ludewa na Mundindi upande wa kaskazini, inapakana na kata na makao makuu ya Wilaya ya Ludewa upande wa maghalibi, inapakana na na Luilo na Nkoma ng’ombe upande wa kusini na mashariki inapakana na Mkoa wa Ruvuma Wilaya ya Mfinga na mto Ruvuma ndio unaotenganisha maeneo hayo kata yenye vijiji 2 vitongoji 7 na inajumla ya wakazi 1643.
Pamoja na kuwa kata hizo zina jumla ya watu zaidi ya 10055 ila bado maisha ya wakazi wake bado ni kuunganisha kutokana na vikwazo mbali mbali wanazozipata katika kujinasua kwenye dimbwi la umasikini.
Katika uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa habari wa mtandao wa jinsia Tanzania (TNGP) katika vijiji hivyo umebaini kwepo kwa safari ndefu kwa serikali kuwakomboa wananchi hao kutoka katika adui umaskini.
Wakazi wa kata ya Ibumi na Mndindi Eleteli Mlelwa na Aletelius Mkolongo wanasema kuwa kutokana na wilaya hiyo ya Ludewa kuwa na utajiri mkubwa wa mchuchuma na liganga hawakutegemea kama serikali ingeendelea kuchelewa kuwafanya wakazi wa kata hizo kuwa na maisha bora .
Anasema Mlelwa kuwa wanashangazwa kuona maisha yanaendelea kuwa magumu katika vijiji vyao huku baadhi ya watoto wa kike na alemavu katika kata yao ya Mndindi wanaendelea kukosa elimu kutokana na umaskini wa familia zao .
“Hivi sasa katika kata yetu wananchi wamekuwa wakifanya jitihada mbali mbali za kujinasua katika dimbwi la umasikini ikiwa ni pamoja na kuongea kasi zaidi ya kilimo lakini bado miundo mbinu mibovu na imekuwa ni chanzo cha wao kuendelea kuwa duni na kuwa na maisha ya kifukara “
Hata hivyo anasema kuwa sehemu kubwa wanaoathirika zaidi na umaskini huo ni wanawake ,watoto na walemavu ambao katika maeneo hayo wamekuwa na kawaida ya kutelekeza familia zao na kukimbilia mijini kwenda kufanya matumizi mabaya ya fedha kidogo wanazozipata katika kilimo.
Mlelwa anasema kuwa ni jambo wa kushangaza kuona watanzania tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru huku wananchi wa vijijini wakiendelea kushuhudia maisha bora kupitia runinga huku katika maeneo yao bado wananchi wakiwa katika gereza la umasikini .
Anasema kuwa bado ni ndoto kwa walemavu na wanawake wa pembezoni mwa Tanzania kuendelea kunufaika na matunda kiasi ya Taifa hili iwapo serikali haitaweka mikakati ya wazi ya kuwakomboa wananchi hao wa vijijini ikiwa ni pamoja na kusogeza masoko ya mazao ,kujenga miundo mbinu bora ya afya ,elimu na usafiri.
Pia anasema kuwa kata yao inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na :
barabara kutopitika karibu wakati wote wa masika na barabara ya mkoa bado ni ya changarawe,ukosefu wa soko la uhakika la mazao ingawa nia mazao ya chakula na ndio kipato cha wananchi wengi vijijini.
Aidha anasema kuwa kata hiyo ya Mndindi inaupungufu mkubwa wa watumishi kwa Idara zote hasa Elimu ya Sekondari hali ni mbaya,Sekondari yetu inapungukiwa majengo muhimu kama maabara hakuna kabisa, ukumbi wa mikutano na mitihani hamna, madarasa hayatoshi nyumba za walimu hazitoshi na mabweni hasa watoto wa kike.
Kuhusu majengo yaliyopo hayana samani kama vitanda, viti meza pia hakuna umeme ingawa ni tatizo la kitaifa, lakini ndani ya Wilaya yetu inarasilimali nyingi mfano mito mikubwa na madini ya mkaa, vinawezesha wananchi wa Ludewa kupata umeme wa kutosha na Inchi nzima,Shule yetu maalumu inamatatizo mengi hasa majengo hayatoshi kulingana na idadi ya watoto waliopo na walimu waliopo hawatoshi.Shule haina muhudumu aliyeajiliwa na ukizingatia na hali ya watoto wanaosoma pale.
Huku afisa mtendaji wa kata ya Ibumi Felix Vichale akidai kuwa huduma za jamii zilizopo ni pamoja na shule za msingi shule Elimu maalumu na Sekondari iliyofikia kidato cha nne mwaka 2010 wakati upande wa afya afya ni zahanati tatu kila kijiji ipo moja.upande wa mawasiliano kata ina barabara za Wilaya za vumbi zinazounganisha kila upande wa kata zinazozunguka kata hii na Barabara ya Mkoa inayoelekea Songea (RUVUMA)
“Wananchi wa kata hii sehemu ni wakulima na wanafanya biashara kiasi, shughuli zao ni kilimo cha mazao ya chakula kama mahindi, maharage, njegele, viazi vitamu, kalanga nk. Na mazao ya biashara ni kahawa, pia wanafuga ngo’ombe wa kienyeji na kisasa kiasi, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, na wanyama wadogo wadogo tuna rasilimali ambazo ni pamoja na ardhi ya kilimo na madini, kata imezungukwa na madini ya chuma, dhahabu na mengine mengi.”
Anasema kuwa wananchi wa kata ya ibumu kwa kujadiliana na wananchi wa kata ya Ludewa, mnamo mwaka 20001 walikubaliana kuanzisha kuchimba barabara kila watu kutoka kwenye kata yao hadi mpakani ambako ni kwenye mto, kata yako kazi hii ilianza mwaka 2002 kwa mkono na serikali Halmashauri ya wilaya pamoja na wafadhili na iliendelea hadi ilipoisha mnamo mwaka 2005.
Barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa 50 ilichimbwa kwa ushirikiano wa wananchi Serikali na wafadhili .
Alitaja wafadhili hao kuwa ni kampuni ya MRMO E.GRANITO ya Mbeya, TASAF na MIMI STEER. Shughuli zilizofanyika ni uchinabji wa barabara hiyo, ujenzi wa makarvati na ujenzi wa madaraja jumla ya gharama katika mradi huu ni karibu TSH milioni 700
Wakati kijiji cha Mavanga kata ya Mavanga kutokana na umasikini wa wananchi wa eneo hilo ambalo linaongoza kwa kilimo cha mahindi ,wameonyesha kushindwa kumalizia majengo ya shule ya msingi Mbugani na kupelekea moja kati ya jingo jipya katika shule hiyo kubomoka kabla ya kuanza kutumika .
Shule hiyo ya Mbugani iliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa zaidi ya shilingi milioni 5 imebomoka baada ya wananchi kukosa fedha za kununua bati na saruji na serikali kushindwa kuunga mkono jitihada hizo
Uongozi wa shule hiyo umesema kuwa kuanguka kwa kuta zote za shule hiyo kumetokana na serikali ya Halmashauri ya wilaya Ludewa kuchelewa kuunga mkono jitihada za wananchi wa kijiji cha Mavanga ambao walilazimika kujitolea kujenga shule hiyo ili kuepusha msongamano wa wanafunzi katika shule moja iliyopo kijijini hapo.
Kaimu mkuu wa shule hiyo Alemaatema Ngalalikwa anasema kuwa shule hiyo imeshindwa kuanza kutokana na jingo moja lenye vyumba viwili vya madarasa kubomoka kwa kukosa bati na saruji na kupelekea shule hiyo kuendelea kusimama bila kupokea wanafunzi.
Hata hivyo alisema kuwa wazo la kujenga mkondo huo mpya wa shule ya Mbugani kulitokana na kikao kilichoketi mwaka 2008 kutathimini tatizo la utoro wa wanafunzi na msongamano wa wanafunzi hao madarasani na kuazimia kujenga majengo hayo.
Alisema kuwa ujenzi huo ulianza toka mwaka 2009 baada ya wananchi kujitolea kufyatua tofali na kusongeza mawe na kuwa mwaka huo huo ujenzi ulikamilika na jumla ya shilingi zaidi ya milioni 5 ndizo zilitumika kujenga majengo hayo ambayo baadhi tayari yamebomoka .
Mbali ya kubomoka kwa majengo hayo pia alisema hata vyumba viwili vya madarasa vilivyosalia katika eneo hilo vipo hatarini kubomoka kutokana na kutosakafiwa kwa saruji na kuwa iwapo serikali itachelewa kusaidia kutoa fedha za kukamilisha ujenzi huo upo uwezekano wa nguvu za wananchi na fedha hizo zaidi ya milioni 5 zilizotumika katika ujenzi huo kupotea.
Pia alisema tatizo la madawati ni kubwa katika shule hiyo mpya ambayo ilitarajiwa kuombewa kibali kwa ajili ya kupunguza wanafunzi kutoka mkondo mama na kuanzishwa kwa shule hiyo na kuwa hadi sasa hakuna dawati hata moja katika vyumba hivyo vya madarasa.
Maria Ngatunga ni afisa mtendaji kata ya Mavanga ambaye alithibitisha kuwepo kwa tatizo la kubomoka kwa madarasa hayo kutokana nna kukosa mchango wa serikali katika kukamilisha ujenzi huo na kuwa kwa sasa tayari Halmashauri iimeazimia kuchangia fedha za kukamilisha ujenzi huo baada ya kutokea kwa maafa hayo ya majengo kubomoka.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe mbali ya kuwapongeza kwa ujenzi wa shule hiyo mpya ambayo kwa sasa majengo yake yameanza kubomoka bado aliahidi kujitolea kuchangia bati 104 ili kuenzeka majengo hayo mara yatakapojengwa upya pamoja na kjmwomba ofisa elimu kuchangia saruji.
Mbunge Filikunjombe anasema kuwa njia pekee ya wananchi hao kukikwamua kiuchumi ni pamoja na kutunza ardhi yao na kuepuka kuuza ardhi kwa wageni ambao wamekuwa wakifika katika maeneo hayo na kutaka ardhi ili kugeuza wilaya hiyo ni sehemu ya kuchuma na kuondoka.
Filikunjombe ambaye kitaalum ni mwanahabari na makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za mashirika ya umma (POAC) anasema kuwa vipaumbele vyake katika wilaya hiyo ni pamoja na kuona ujenzi wa barabara ya lami unaanza katika wilaya ya Ludewa ambayo kwa sasa haina hata robo kilometa ya lami na kipaumbele cha pili ni uchimbaji wa makaa Liganga na mchuchuma.
Anasema kuwa tatizo la umasikini wa wananchi katika wilaya ya Ludewa ni pamoja na rasilimali za wilaya hiyo kushindwa kutumika vema na kuwa iwapo rasilimali hizo zitatumika vema milango ya umasikini kwa wananchi wa vijiji vya wilaya hiyo itafungwa na kufunguliwa ile ya uchumi.
Imeandaliwa na Francis Godwin mwenyekiti wa waandishi wa habari wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) mikoa ya kusini mwa Tanzania na mmiliki wa mtandao huu na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima mkoa wa Iringa.

No comments: