Mbunge wa Munduli, Edward Lowassa(Katikati)akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma jana, walipotaka kupata maoni yake kuhusu uamuzi wa Rostam Aziz kujiuzulu nyadhifa zake za ubunge wa Igunga na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM hata hivyo Edward Lowassa ameeleza kushtushwa na tukio hilo.
Hata hivyo, Lowassa ambaye naye amekuwa akitajwa katika orodha ya watu watatu wanaopaswa kuachia nafasi zao za uongozi CCM katika kile kinachoitwa chama kujivua gamba, alipoulizwa kuhusu taarifa za yeye kufuata njia ya mshirika wake huyo alijibu: 'Siku ikifika nitatoa uamuzi na nitajibu wakati ukifika.'
Lowassa alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma, kuhusu alivyopokea uamuzi huo wa Rostam na kama yuko tayari kufuata mfano na njia hiyo ya kujiuzulu nyadhifa zote ndani ya CCM.
No comments:
Post a Comment