Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, July 7, 2011

Mfuko wa PSPF Wapongezwa kwa Kutoa Mafao Bora Zaidi ya Pensheni-Mkulo

Waziri wa Fedha, Mhe. Mustafa Mkulo, akisaini kitabu cha wageni, alipolilitembelea banda la PSPF kwenye maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, ambapo Mfuko huo, umehamishia baasdhi ya huduma zake, kwenye banda lake la sabasaba.
Mwanachama wa PSPF akishangalia modeli ya nyumba za kisasa za gharama nafuu ambazo mfuko huo umejipanga kuwauzia. Modeli ya nyumba hizo, zimekuwa kivutio kikubwa kwenye banda la PSPF kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.
Wanachama wa PSPF wakishangalia modeli ya nyumba za kisasa za gharama nafuu ambazo mfuko huo umejipanga kuwauzia. Modeli ya nyumba hizo, zimekuwa kivutio kikubwa kwenye banda la PSPF kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.
Wanachama wa PSPF wakihudumiwa kwenye banda la PSPF ambapo mfuko huo, umehamishia baadhi ya huduma zake kwenye banda hilo.
Mwanachama wa PSPF akishuhudia mkokotoo wa mafao yake yote pindi atakapo staafu. Mkokotoo huo, umefuatia maofisa wa PSPF kumkokotolea mafao yake kwenye banda la PSPF kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

===== ===== ====== ====== ====== ======
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, PSPF, umepongezwa kwa kuwa ndio mfuko unaotoa mafao bora zaidi kwa wanachama wake, kuliko mifuko mingine yote, kufuatia mfuko huo kuanzisha mpango wa kujenga nyumba za gharama nafuu na kuwauzia wanachama wake.

Pongezi hizo, zimetolewa jana, na Waziri wa Fedha, Mhe. Mustafa Mkulo, alipolilitembelea banda la PSPF kwenye maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, ambapo Mfuko huo, umehamishia baasdhi ya huduma zake, kwenye banda lake la sabasaba.

Waziri Mkulo amesema, kufuatia mafao bora ya uzeeni yatolewayo na mfuko huo, Watumishi wa Umma, wanaishi kifua mbele hata baada ya kustaafu.Mkuu wa Banda la PSPF, Fatma Elhady, amesema PSPF iko katika mchakato wa kupanga utaratibu wa kufuatwa na wanachama wa mfuko huo ili waweze kuzinunua nyumba hizo. 
 Habari kwa Hisani ya Jiachie Blog

No comments: