hivi ndivyo hali ilivyotokea baada ya basi la Hood lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Arusha,lilipogongana uso kwa uso na lori la mizigo lilolokuwa na mafuta ya kula tani 24 kutoka Morogoro kwenda Songea jana kwenye barabara iliyopo ndani ya hifandi ya Taifa ya Mikuki,mkoani Morogoro.watu watano walifariki na 41 kujeruhiwa.
Moto mkali ukiwaka mara baada ya magari hayo kugongana.
Basi la Hood lionekanavyo mara baada ya kuteketea kwa moto.
Dereva wa basi la Hood, Salehe Tembo ( 42) mkazi wa Mbezi , Jijini Dar es Salaam, akiwapelekwa chumba cha X –Ray kwa ajili ya kupigwa picha kabla ya kupatiwa matibabu baada ya kuungua sehemu mbalimbali mwilini.
Mama Asha Maneno akiwa na mwanae Milka Maneno , wakazi wa Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wodini baada ya kuumia sehemu mbalimbali za miili yao , katika ajali ya basi la Hood lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Arusha lilipogongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mafuta, eneo la mbunga ya wanyama ya Mikumi. Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.
Habari kwa Hisani ya Issa michuzi
No comments:
Post a Comment