BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI ILIYOWASILISHWA NA WAZIRI WILLIAM NGELEJA LEO HUKO BUNGENI DODOMA IMEKATALIWA NA WAHE. WABUNGE NA WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA AMEOMBA SERIKALI IPEWE WIKI TATU KUIREKEBISHA NA KUIRUDISHA ISOMWE UPYA.
SPIKA WA BUNGE MHE. ANNE MAKINDA AMEAFIKI KUKATALIWA KWA BAJETI HIYO AKIITA NI NYETI NA KUSEMA ITAPOKUJA KUSOMWA TENA IWE NA MAJIBU YA UHALISIA NA MIPANGO INAYOTEKELEZEKA.
HII NI MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA BUNGE LA NCHI HATUA HII KUFIKIWA, INGAWA HUKO NYUMA BAJETI KAMA MBILI ZILIONDOLEWA KABLA YA KUSOMWA .
WENGI WALITEGEMEA KWAMBA WAZIRI NGELEJA KUKAANGWA ILE MBAYA, ILA SIO KUKATALIWA KWA BAJETI NZIMA NA KUTAKIWA IANDIKWE UPYA ILI KIELEWEKE.
HABARI KAMILI BAADAYE
HABARI KWA HISANI YA ISSA MICHUZI
No comments:
Post a Comment