Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, July 18, 2011

Anaedurufu kanda za wasanii wa muziki wa injili adakwa jijini dar

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki baada ya kumkamata mmoja wa watuhumiwa wa mtandao wa kundi la wanyonyaji wa kazi za wasanii wa muziki wa injili, Mwakwi Yahya. Hivi karibuni pia alikamatwa, Francis Kamalamu aliyekuwa akifanya biashara hiyo eneo la Ubungo Maziwa, Dar es Salaam.
Mtuhumiwa aliyekamatwa kwa kurudufu kanda, Mwakwi Yahya mkazi wa Mabibo, Dar es Salaam, akionesha kanda hizo kwenye Kituo cha Polisi Urafiki.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Msama Promotions, imemkamata mmoja wa watuhumiwa wa mtandao wa kundi la wanyonyaji wa kazi za wasanii wa muziki wa injili, Mwakwi Yahya.

Mtuhumiwa huyo aliyekamatwa mwishoni mwa wiki kwa kurudufu kanda ambaye ni mkazi wa Mabibo, Dar es Salaam, alipelekwa Kituo cha Polisi Urafiki.

Kukamatwa kwa Yahya kimetokea siku chache baada ya kiongozi wao, Francis Kamalamu, aliyekuwa akifanya biashara hiyo katika eneo la Ubungo Maziwa, Dar es Salaam, naye kutiwa mbaroni.

Harakati za kumkamata kiongozi huyo zilianza mwanzoni mwa wiki iliyopita, ambapo maofisa usambazaji wa Kampuni ya Msama Promotions, walianza harakati za kuwasaka wanyonyaji hao na kufanikiwa kumnasa kijana huyo akiziuza CD za muziki wa Injili katika eneo hilo.

Baada ya kuzikuta, maofisa hao walijifanya ni wateja wa CD hizo na kumtaka kijana huyo awatafutie CD 150, ili wao wakaendeleze biashara hiyo, ambapo kijana huyo aliwaeleza kuwa kuna mtu anayeifanya kazi ya kunyonya kazi hizo na kuahidi kuwapeleka kwa mhusika ili wafanikishe kazi yao.

Mtuhumwia huyo alipokutana na maofisa wa Msama Promotions, aliwataka wateja wake hao kurejea mwishoni mwa wiki iliyopita ili kuwakabidhi mzigo wao, ambapo bila kuonesha dalili za kutaka kumkamata, walikubali ombi lake.

Mtego huo ulikamilika kwa maofisa wa kampuni hiyo wakishirikiana na Polisi kufanikisha lengo la kumtia nguvuni mnyonyaji huyo.

Imeelezwa kuwa baada ya mahojiano marefu mtuhumiwa alieleza kuwa alikuwa akiiuza CD moja kwa sh. 1,700, na alikuwa na albamu za Haleluya Collection, Shengena na albamu ya mtu wa nne. Alikuwa na nakala zaidi ya 100.

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akijikusanyia zaidi ya sh. milioni 2.1 kutokana na kunakili muziki huo.

Mtuhumiwa bado anaendelea kushikiliwa kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela, alisema uchunguzi zaidi unaendelea

No comments: