Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, June 2, 2011

Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania walivyosherehekea siku ya watoto yatima kituo cha Kurasini

  Mtoto Nyambu Jumanne wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam akichezea kifaa cha kukimbiza upepo alichopewa na Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania. Wachina hao walisherehekea siku ya mtoto jana pamoja na watoto yatima wa kituo hicho na kuwapatia zawadi  mbalimbali zikiwemo nguo, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, viatu, madawa na vifaa vya kuchezea.

Mtoto  He Yu Chi (Kushoto) kutoka  Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania akimkabidhi mtoto Bakari Majuto (kulia) wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam zawadi za nguo. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea.

Xu Wu  (Kushoto) kutoka  Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania akimkabidhi nesi Eulelia Michael  (kulia) kutoka kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam maboxi yenye dawa za kutibu ugonjwa wa maralia kwa watoto . Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, viatu, madawa na vifaa vya kuchezea.

 Guo Li (kushoto) kutoka  Jumuia ya  wachina waishio nchini Tanzania akimkabidhi Margaret Mkandawire (kulia) ambaye ni Mkuu wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini  jijini Dar es Salaam zawadi za mabegi ya shule na miamvuli kwa ajili ya watoto wa kituo hicho. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, vyakula, masanduku ya kuwekea nguo viatu, madawa na vifaa vya kuchezea

 Mtoto Amina Said (kulia) wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini  jijini Dar es Salaam akijaribu zawadi ya kandambili aina ya yeboyebo alizopewa na jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania.Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, masanduku ya kuwekea nguo ,viatu,vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea.

Margaret Mkandawire (kulia) ambaye ni Mkuu wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini  jijini Dar es Salaam akiwa katika picha ya pamoja na Wu Quan Shengi (katikati) na Xu Wu (kushoto) kutoka jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania mara baada ya kukabidhiwa zawadi za mipira kwa ajili ya watoto wa kituo hicho. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea.

Xu Wu  (Kulia) kutoka  Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania akiwakabidhi mikebe ya shule baadhi ya watoto  kutoka kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea.

Baadhi ya wachina kutoka Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania wakiwa na watoto  kutoka kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuwagawia zawadi. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea.

Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watoto  pamoja na walezi kutoka kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea.

Watoto kutoka kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam wakimba wimbo wa kuelezea jinsi wazazi wanavyowatelekeza watoto wao wakati Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania walipowatembelea . Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea.

 Bai Ling Bo ( wa tatu kushoto) kutoka  Jumuia ya  wachina waishio nchini Tanzania akimkabidhi Margaret Mkandawire (kulia) ambaye ni Mkuu wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini  jijini Dar es Salaam zawadi za kuchezea watoto wa kituo hicho. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, vyakula, masanduku ya kuwekea nguo viatu, madawa na vifaa vya kuchezea.

Yu Xiu Mei (kushoto) kutoka  Jumuia ya  wachina waishio nchini Tanzania akimkabidhi Margaret Mkandawire (kulia) ambaye ni Mkuu wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini  jijini Dar es Salaam zawadi za masanduku ya kuwekea nguo kwa ajili ya watoto wa kituo hicho. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, vyakula, masanduku ya kuwekea nguo viatu, madawa na vifaa vya kuchezea.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo

No comments: