Benki ya CRDB imepata faida ya Tsh bilioni 66 Kabla ya kodi, hilo lilisemwa jijini Arusha na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Bw. Martin Mmari katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa wa Benki hiyo. Bw.Mmari alisema hili ni ongezeko la asilmia 7 kutoka Tsh 62 bilioni zilizopatikana mwaka 2009. Kutoka na ongezeko hilo Bw. Mmari alisema gawio la hisa limeongezeka mpaka kuwa Shilingi 8 kwa kila hisa. Bw. Mmari alisema kuwa pamoja na faida hiyo Benki CRDB itaendelea na sera yake ya kutumia asilimia moja ya faida yake katika kuisadia jamii yaani "Corporate Social Responsibility''.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa wazamani Mh. Fredrick Sumaye alishinda kwa kishindo na kupata nafasi ya kuwa mjumbe wa Bodi wa Benki hiyo katika uchaguzi wa wanahisa uliokuwa sehemu ya mkutanO huo.Bwana Sumaye alipata asilimia 60 ya kura zote na kuwabwaga wanahisa wengine 23 waliokuwa wakiwania nafasi hiyo. Akizungumzia ushindi huo Bw.Sumaye alisema "Mimi kama Mtanzania na mwanahisa wa Benki ya CRDB nimeona ni muhimu kuongeza nguvu na uzoefu wangu katika kuendeleza zaidi Benki yetu
Katibu wa Benki ya CRDB Bw.John Rugambo akimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Fredrick Sumaye kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe mpya wa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo katika mkutano mkuu wa wanahisa uliofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC mjini Arusha. Kushoto ni mwenyekiti wa Mkutano huo Bw.Damian Ruhinda na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki hiyo Bw.Martin Mmari.
Habari kwa hisani ya Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment