Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, May 31, 2011

shilingi bil. 2.5 zatumika kulipa fidia wakazi wa GEZAULOLE

Mstahiki Meya wa wilaya ya Temeke (kulia) Maabad Hoja akiingia katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za manispaa ya Temeke kwa ajili ya kuanza kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika leo.
Baadhi ya madiwani wa wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa umakini majibu ya maswali yaliyokuwa yanajibiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Eng.Gaston Gasama (hayupo pichani) wakati wa kikao chao kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo manispaa ya Temeke.
Baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo wa wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa umakini majibu ya maswali yaliyokuwa yanajibiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Eng.Gaston Gasama wakati wa kikao chao kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo manispaa ya Temeke.
Madiwani wa wilaya ya Temeke wakiwa katika kikao chao leo kinachofanyika kila baada ya miezi katika ukumbi wa mikutano uliopo manispaa ya Temeke.Picha na Anna Nkinda - Maelezo


Na Magreth Kinabo – Maelezo

Shilingi bilioni 2.5 zimetumika kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi 313 kati ya 427 kwenye mradi wa upimaji viwanja Gezaulole wilayani Temeke.

Hayo yamesemwa leo na ofisa mipango miji wa manispaa ya Temeke Photidas Kagimbo wakati akitoa taarifa ya maendeo ya mradi huo katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo.

“Zoezi hili linaendelea vizuri hadi kufikia jana tumeshalipa fidia ya shilingi bilioni 2.5 kati ya shilingi bilioni 2.8 zinazotakiwa kulipwa fidia kwa wananchi hao ambao ni sawa na asilimia 79,” alisema Kagimbo.

Aliendelea kusema kuwa maradi huo ambao ni wa awamu ya kwanza unajumla ya viwanja zaidi ya 700 na tayari zoezi la uchukuaji fomu limeshakamilika jana ambapo urudishwaji wake mwisho ni ijumaa ya tarehe 3 mwezi wa sita mwaka huu.

Kagimbo alifafanua kuwa mradi wa awamu ya pili uko katika mchakato na tayari fedha za fidia za kuwalipa wananchi zimeshatengwa ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni sita.

Alisema, “Kabla ya kufikia mwishoni mwa mwaka huu tunatarajia kupima viwanja zaidi ya 4000 katika eneo la Gezaulole na mara baada ya kukamilika kwa zoezi hili tutawajulisha wananchi ili waweze kutuma maombi kwajili ya kupatiwa viwanja.”

Mradi huu ulianza mwaka 2007 lakini ulisimama kutokana na ufinyu wa bajeti kwa ajili ya upimaji na ulipaji wa fidia kwa wananchi hivi sasa mradi huo unaendelea baada ya manispaa hiyo kupata fedha za mkopo kutoka Benki ya Rasilimali (TIB) na wizara ya Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi.

No comments: