Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, May 1, 2011

sherehe za mei mosi jijini dar leo

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Ilala jukwaa kuu wakati akipokea maandamano ya wafanyakazi katika sherehe hizo.
Gari la Maliasili likipita huku likiwa na mapambo ya ngozi za wanyama wakali kama Chui na wengineo katika maadhimisho hayo.
Askari wa Jeshi la Magereza wakiongoza maandamano hayo kuelekea ndani ya Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Wafanyazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, akiwemo Mwanalibeneke Muhidin Sufiani (aliening'iniza miwani shingoni) wakishiriki katika maandamano hayo kuelekea Viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani.
Maandamano yakiendelea kuelekea Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Wafanyakazi wa Tawi la Kampuni ya Tuico, wakipita mbele ya Jukwaa kuu na mabango yao yenye Ujumbe, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo na kuhudhuliwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Mecky Sadiki. Sherehe hizo zimefanyika kitaifa mkoani Morogoro ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya kikwete.
Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakipita jukwaa Kuu huku wakishangilia na kufurahia, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana na kuhudhuliwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki. Sherehe hizo zilifanyika kitaifa mkoani Morogoro ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya kikwete.Picha na Muhidin Sufiani wa Ofisi ya Makamu wa Rais.
Picha na maelezo kwa hisani ya Issa Michuzi Blog

No comments: