Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza wakati akisoma hotuba yake ya uzinduzi rasmi wa Mfuko wa kusaidia Wazee wasiojiweza wa ‘Pamoja Tushikamane’ ulio chini ya Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tushikamane Pamoja Faundation. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana Mei 24.
Mmoja kati ya wageni waalikwa, Bi. Eshe Sururu, akizungumza kutangaza kiasi alichotoa kuchangia mfuko huo jana, ambapo alitangaza kuchangia Sh. 500.000.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (katikati) na Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tushikamane Pamoja Faundation, Rose Mwapachu (kulia) wakipiga makofi kuwashangilia watu waliojitolea kuchangia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfuko huo iliyofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam jana Mei 24.
No comments:
Post a Comment