Mtoto Hamisi akiwa yuko na Ng'ombe kibao katika mbuga moja huko Mbeya Vijijini
Mtoto Hamisi akijitahidi kuzuia mifugo hiyo isipate kula Mahindi na na Maharage katika shughuri zake za kuchunga
Hawa ni mifugo wengine ambao wanachungwa na mtoto John
Mtoto John akiwa anasikia Njaa vibaya mida ya saa nane mchana huko maporini huku asijue atapata chakula mida gani.
Ilikua ni mida ya sa Saba mchana ambapo timu yetu ilikua maeneo ya Mbeya vijijini kuona mambo mawili matatu yanavyo endelea kufanyika, na ndipo tulifika kijiji kimoja na kustaajabu kuona watoto wadogo wenye umri wa kwenda darasa la tatu na la nne wakiwa maporini wanachunga mifugo huku wakiwa na Njaa kali. Tulipata nafasi ya kufanya nao mahojiano kila mmoja kwa wakati wake na hivi ndivyo mtoto Hamisi alizungumza "Mimi baba hataki nisome,aliniachisha shule ili nije kuchunga hawa mifugo. Nilimuomba sana Baba niendelee na shule lakin amegoma kabisa kwa hiyo ndio nipo nafanya kazi hii ingawa siipendi sana na nampango wa kutoroka nyumbani, nateseka sana kwa sababu nikitoka asubuhi sili mpaka sa kumi na mbili napo Rudisha mifugo nyumbani" hata hivyo tulipo muhoji zaidi hakujibu kitu na kusema ndio hayo tuu. kwa upande wa pili nae mtoto John alikua na haya ya kusema "Mimi naitwa John kusema ukweli wazazi katika kijiji hiki hawapendi watoto waende shule kwa kusingizia kuwa walimu wanatupa kazi nyingi sana, sasa ili kupunguza kazi hizo na kuweka sawa ndio maana wanatuachisha shule tupate chunga hii mifugo, hii ni kazi mbaya sana kwa sababu siku zote tunashinda na njaa hata hapa nimeokota tunda ndo nilalila baadae nipunguze njaa yangu" aliongea John huku akiendelea kuwachinga mifugo hao.
Swali ambalo tunatakiwa kujiuliza watanzania wenzetu ni kwamba je Haya mambo ya kuwanyanyasa watoto kama hawa wadogo yataisha lini? Na wanao husika na haki za watoto hatupii macho yao Vijijini?
No comments:
Post a Comment