Na Nafisa Madai,MAELEZO Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekata mzizi wa fitina juu ya Mradi mkubwa wa ujenzi wa Hoteli yenye hadhi ya nyota tano katika eneo la Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Kampuni ya Zamani Zanzibar Kempinski imo katika hatua za mwisho kujenga Hoteli hiyo baada ya kukamilisha taratibu zote Serikalini ikiwa pamoja na kufuata na kuzingatia sheria za uhifadhi na uendelezaji wa Mji Mkongwe unaolindwa Kimataifa.
“Kama kuna watu wanataka kwenda Mahakamani kupinga ujenzi waache wende, lakini uamuzi wa Serikali utabaki pale pale kwamba ujenzi wa hoteli iliyokusudiwa utaendelea” Alisema Dk Shein katika mkutano na waandishi wa habari jana usiku.
Dk Shein alifanya mkutano huo na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kurejea kutoka ziara ya Kiserikali nchini Uturuki ambapo katika mahojiano, aliulizwa swali juu ya pingamizi inayokusudiwa kuwekwa kuzuia ujenzi wa mradi wa Hoteli na msimamo wa Serikali.
“Ile ni mali yetu hakuna wa kutuzuia na nataka kusema kuwa hili jambo Serikali imeamua, sasa sioni tatizo liko wapi kwani mtu ukiamua kuuza chake nani atakuzui…hakuna” Alisisitiza.
Juma Ali Khatib na wenzake, wanakusudia kuishtaki Serikali kupinga ujenzi wa hoteli hiyo wakidai utaratibu wa uuzaji wa mali za umma umekiukwa.
Vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya Serikali vinaeleza Kampuni ya Kempinski imelipa bilioni 2 milioni 880 kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na fedha hizo kuwekwa katika hazina ya Serikali.
Chini ya mradi huo, Kampuni Kempinski inatarajia kuwekeza kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 30 ambazo zitahusisha ukarabati wa jengo la kihistoria la Mambo Msiige, ujenzi wa bustani ya kisasa na hoteli yenye hadhi ya nyota tano itakayojengwa ilipokuwa starehe klabu.
Utaratibu ukodishwaji wa ardhi kwa mgeni Zanzibar hekta moja ikiwa sawa na eka 2.4 inakodishwa kwa Dola za marekani 5000 kwa mwaka ambapo Kempinski eneo alilokodishwa halijafikia hata eka moja wamekodishwa kwa Dola 10,000 kwa mwaka.
Wakati Kempinski ikilalamikiwa, kuna Taasisi zimekodishwa majengo ya umma kwa bei ya kutupa ikiwemo Aga Khan Development iliyokodishwa Jumba la Kihistoria la Mawasiliano ya Simu kutoka Aden (sasa Serena Inn).
Jengo hilo analipia sh. milioni moja kwa mwaka na jengo jingine katika Mji Mkongwe la Old Dispensary iliyokuwa mkabala na mgahawa wa Mercury ambalo analipa dola moja ya Marekani kwa mwaka.
Mbali na mali hizo, Taasisi hiyo ilipewa hekta 75 za ardhi katika Kijiji cha Mangapwani mkoa wa Kaskazini Unguja ambalo kwa zaidi ya miaka 20 sasa bado halijaendelezwa, kiasi cha kufanya Serikali kulipunguza na kuibakizia eka 20 ambazo amejenga mgahawa na nyingine wamepewa wananchi.
Mwekezaji mwingine S.S. Bakhressa kwa ushauri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, amekodishwa jengo lililokuwa likitumiwa na wizara hiyo Mji Mkongwe, kwa ajili ya mradi wa hoteli ya kitalii ambapo amelipa dola milioni 1.5.
Rais Dk Shein amewahakikishia wananchi kwamba miradi hiyo itazingatia sheria za uhifadhi na uendelezaji wa Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao unatambuluwa kuwa ni urithi wa ulimwengu na UNESCO.
Nchini Tanzania kampuni ya Kempinski imewekeza katika miradi mikubwa ya hoteli za kitalii zenye hadhi ya nyota tano ikiwemo Zamani Zanzibar Kempinksi,Bilila Lodge Kempinski Serengeti,Hotel Ngorongoro Kempinski na Kilimanjaro Hotel Kempinski Dar es Salaam.
Habari kwa hisani ya Michuzi Blog

No comments:
Post a Comment