Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, May 5, 2011

Adha ya Mifereji maji chafu maeneo ya Sinza makaburini

Maji taka yamekwama huku upande wa juu huduma za kijamii zinaendelea kama kawaida
Mfereji wa maji Taka na juu bomba la maji safi limekatiza 
Katika hali isiyo ya kawaida muda huu Kamera yetu imepita maeneo ya Sinza Makaburini na mfereji wa maji taka huku juu yake kuna Bomba la maji safi linakatiza, maji hayo machafu ambayo yametwama katika mfereji huo ambao upo bara  barani kabisa unatoa harufumbaya na kusababisha Kero kwa wakazi waishio maeneo hayo. Hata hivyo juhudi zimefanyika kuwatafuta wakazi wa eneo hilo husika,wamedai kuwa walisha lalamika sana lakini wahusika wamefumbia macho na kuziba masikio.

Wanachi hao waliendelea kulalamika sana na mmoja wao aliacha swali lake tunamnukuu "Sasa mimi naomba kuwauliza hawa wahusika wa kuzibua mifereji ya maji taka kama ndio hii adha ingewapata milangoni katika nyumba zao wangefumbia macho?"

No comments: