Kwanza tunapenda sana Kuwashukuru watanzania wote kwa kuipokea Radio yenu vema, na kwa kutambua umuhimu wenu tumekuwa tukifanya kila liwezekanalo ili tupate kuwafikia popote Duniani. Pili tunaomba Radhi sana kwa usumbufu wowote ambao umejitokeza Radio kuwa On Air na Off Air, hata hivyo tunapenda kuwataarifu ya kuwa Radio yenu Bora Haitakuwa On Air kwa Muda wa siku Chache kwa sababu za kiufundi na maboresho makubwa yanayo endelea kufanyika kwa sasa Hivyo tunawaomba muendelee kuvuta subira, Hata hivyo bado Radio iko hewani mnaweza kuendelea kupata Burudani Zaid na Zaidi kwa Vipindi vyetu ambavyo tayari vipo hapo na pia Burudani zaid na Muziki wa aina yake.
Uongozi mzima wa Tanzania Online Internet Radio wakiwemo Victor Luvena, Danny Tweve, Joseph Mwaisango,Luseshelo Ernest Njeje,Sillah Mbuya na Fredy Anthony Njeje tunaenda kuchukua nafasi hii kuwashukuruni sana, na tegemeeni mambo makubwa hivi karibuni.
Asanteni sana
Utawala
No comments:
Post a Comment