Bw. Abdalla Zombe akidai chake
Ikiwa ni takriban mwaka mmoja na nusu tangu kuachiwa huru baada ya kushinda kesi, aliyekuwa mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa Madini kutoka Mahenge Morogoro na dereva taksi mmoja wa jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi (ACP) Abdallah Zombe amefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuishtaki Serikali.
Zombe anaiomba Mahakama iamuru Serikali imlipe fidia ya jumla ya Sh bilioni 5.2, ambapo anadai kiasi hicho ni fidia ya madhara ya jumla aliyoyapata kutokana na kesi ya hiyo, au kiasi chochote ambacho Mahakama itaona kinafaa na Sh milioni 200 ikiwa ni fidia kwa adhabu ya kumweka ndani, riba pamoja na gharama za kesi hiyo.
Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa na Wakili wake Richard Rweyongeza wa kampuni ya uwakili ya RK Rweyongeza&Co. Advocates, Zombe anadai alipwe fidia ya kiasi hicho kutokana na madhara aliyoyapata kutokana na kesi hiyo kwa kosa la kukamatwa na kumshtaki kwa tuhuma hizo akidai kuwa ni ukiukwaji wa sheria.
Katika kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2011, Zombe mbali na kuomba Mahakama iiamuru Serikali imlipe fidia ya kiasi hicho, pia anaomba Mahakama hiyo itamke kuwa alikamatwa na kushtakiwa kinyume cha sheria.
Zombe anadai kuwa kabla ya kukamatwa alikuwa amehamishiwa katika Mkoa wa Rukwa na alirejeshwa makao makuu ya Polisi siku 14 baada ya kuwa ameripoti katika kituo chake hicho kipya cha kazi.
Anadai kuwa siku hiyo kabla ya kukamatwa na kupandishwa kizimbani aliitwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ambaye alimjulisha kuwa anatakiwa kuunganishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo.
Anadai kuwa baada ya taarifa hizo alichukuliwa ghafla na kupelekwa mahakamani ambapo Hakimu Mkazi Mkuu alikuwa akimsubiri na kwamba mara baada ya kusomewa
mashtaka yake alipelekwa katika gereza la Ukonga mahali ambako kila kitu kilikuwa kimeandaliwa kwa ajili ya kumpokea.
Lakini analalamika kuwa baada ya kukamatwa polisi walikuwa na wajibu wa kumuuliza kama alikuwa na jambo lolote la kusema ikiwa ni pamoja na kuweka
kumbukumbu zake maelezo yake.
kumbukumbu zake maelezo yake.
Kwa mujibu wa hati hiyo Zombe anadai kuwa kinyume chake kukamatwa kwake kulifanyika kinyume cha wajibu huyo uliotajwa hapo juu na bila kusikilizwa mlalamikaji kama alikuwa na cha kusema kuhusu ushiriki wake katika tuhuma hizo zinazomkabili.
Anadai wakati akiwa mahabusu katika gereza la Ukonga na
baadaye Keko, Zombe aliwasilisha malalamiko yake kwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya kisheria jinsi alivyotendewa lakini hakupata mrejesho wowote kutoka
kwa Waziri huyo.
baadaye Keko, Zombe aliwasilisha malalamiko yake kwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya kisheria jinsi alivyotendewa lakini hakupata mrejesho wowote kutoka
kwa Waziri huyo.
Analalamikia pia polisi kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria na kutokupewa haki ya kujieleza kama mtuhumiwa na matokeo yake kushtakiwa bila
ushahidi wowote wa kumuunganisha katika tuhuma hizo.
Zombe anadai kukamatwa na kushtakiwa kwake kulifanywa kama matokeo ya Polisi kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria waliopewa chini ya sheria za nchi.
Anadai kuwa kwa kuwa alikuwa na uelewa wa matakwa ya sheria alijeruhiwa sana kiakili na kupata usumbufu ambapo alifedheshwa na aliathirika kwa maumivu ya kiakili kutokana na mchakato mzima wa mashtaka kwa jinsi ulivyoendeshwa.
”Polisi kwa makusudi waliacha kuchukua maelezo ya mlalamikaji kuepuka uchunguzi linganifu ambayo yangewezesha kumuachia kabla ya kufikishwa mahakamani, kosa ambalo mteja wangu anadai fidia ya Sh milioni 200 kwa madhara aliyopata.
”Polisi kwa makusudi waliacha kuchukua maelezo ya mlalamikaji kuepuka uchunguzi linganifu ambayo yangewezesha kumuachia kabla ya kufikishwa mahakamani, kosa ambalo mteja wangu anadai fidia ya Sh milioni 200 kwa madhara aliyopata.
“Kama matokeo ya Polisi kushindwa kutimiza wajibu wake na madhara yaliyompata mlalamikaji, sasa anadai fidia ya Sh bilioni 5 kwa madhara ya jumla au kiasi chochote kadri mahakama itakavyoona inafaa,” inadai sehemu ya hati hiyo ya madai.
Sanjari na madai hayo ya fidia, pia Zombe katika hati hiyo ametoa utetezi wake kuhusu tukio la mauaji hayo aliyohusishwa akianza na historia yake tangu alivyojiunga na jeshi hilo na kupanda vyeo na nyadhifa alizotumikia hatua kwa hatua, kabla ya kukumbwa na tuhuma hizo.
Anadai kuwa alijiunga na jeshi hilo mwaka 1977 akiwa na cheo cha Konstebo huku akijinasibu kuwa alifanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa na kwa kujitoa na kupanda katika vyeo mbalimbali hadi alipofikia cheo cha ACP Juni 25, mwaka 2003.
Anadai kuwa Julai 2001 alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) na kwamba Julai 2, mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.
Anasema kabla ya kwenda kuripoti aliyekuwa RPC wa Dar es Salaam alikuwa likizo hivyo yeye akawa anakaimu nafasi hiyo wakati huo pia akiwa bado anafanya kazi kama RCO.
Anaeleza kuwa wakati akiendelea na wadhifa huo, Januari 14, 2006, watu wanne waliuawa na mauaji yao yalihusishwa na askari polisi na kwamba yeye alijulishwa kuhusu tukio hilo na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa Kinondoni.
Anadai kuwa Januari 30 ,2006 alikabidhi madaraka aliyokuwa akitumikia na aliyokuwa akikaimu kisha Februari 2, mwaka huo akaondoka kwenda katika kituo chake kipya kutumikia wadhifa wa RPC mkoani Rukwa.
Anabainisha kuwa kabla ya kwenda Rukwa, Rais alikuwa ameunda Tume ya kuchunguza tukio la mauaji hayo na kwamba ingawa na yeye alihojiwa na tume hiyo
lakini haikupendekeza akamatwe na kushtakiwa.
lakini haikupendekeza akamatwe na kushtakiwa.
Anasema tume hiyo badala yake ilipendekeza askari 15 tu kukamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za mauaji hayo, lakini siku 14 baadaye baada ya kuwa ameripoti Rukwa alirudishwa Dar es Salaam na kupangiwa kazi makao makuu ya jeshi hilo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Zombe anadai Juni 9, mwaka 2006 aliitwa katika ofisi ya IGP na kutii ambapo alimtaarifu kuwa anatakiwa kuunganishwa na washitakiwa wengine wanaotuhumiwa
kuwaua watu wanne .
kuwaua watu wanne .
Hata hivyo, wakati wakati Zombe akifungua kesi hiyo dhidi ya Serikali, bado kuna rufaa iliyokatwa na Serikali Mahakama ya Rufani kupinga hukumu iliyomwachia huru yeye na wenzake nane, ambayo bado haijatolewa uamuzi wala kusikilizwa
Zombe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza Juni 9 mwaka 2006 na kuunganishwa na askari wenzake wengine walikuwa 13 wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya wafanyabiashara hao.
Zombe na wenzake alikuwa wakidaiwa kuwaua wafanyabiashara hao wa madini Sabinus Chigumbi (Jongo), Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi Juma Ndugu, katika msitu wa Pande wilayani Kinondoni nje kidohawana hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.NA MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment