Ushuhuda wa ‘waliopona’ utata mtupu
NI majira ya saa ya tano asubuhi. Nawasili nyumbani kwa Mchungaji Mstaafu Ambilikile Nasapila (76) “Babu” iliyopo katika kijiji cha Samunge, tarafa ya Sale, Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha, umbali wa Kilometa kama 400 kutoka mjini Arusha baada ya safari ndefu ya saa zaidi ya nane.
Kwa hakika, kijiji hiki kwa sasa ndicho kijiji kinachotajwa sana na watu kuliko kijiji kingine chochote mkoani Arusha kama si Tanzania baada ya mchungaji huyo ‘kugundua’ kinachoitwa kuwa ni “dawa ya ajabu” inayotibu maradhi sugu matano.
Safari yetu ilianza saa usiku wa Alhamisi ya Machi 3 kwa gari aina ya Landcruiser lenye namba za usajili T 612 AGP likiendeshwa na dereva Victor Leons, na kwa hakika safari hiyo imeacha kumbukumbu ya aina yake kwa kuwa moja ya safari ngumu sana baada ya gari letu kupata hitilafu ya kupasuka kwa rejeta kabla ya kufika kijiji cha Engaruka wilayani Monduli.
Wakati gari linapata hitilafu ilikuwa imetimu saa 10 za alfajiri na mimi na abiria wengine wanane niliokuwa nasafiri nao, tulilazimika kusubiri usiku huo katikati ya pori ambalo linaelezwa kuwa na wanyama wakali hadi tulipopata msaada wa msamaria mwema mmoja aliyekuwa akipita barabara hiyo ambaye alitusaidia majani ya chai na maji kiasi cha lita 5 ambayo tuliyatumia kuyaweka katika rejeta hiyo kuziba sehemu iliyotoboka.
Wahenga walisema msafiri kafiri. Ni baada ya “sayansi” hiyo isiyo rasmi ya ‘kutibu’ gari ndipo tulipoendelea na safari na kufika kijiji cha Engaruka ambako tulinunua madumu yenye maji na majani ya chai ya kutosha na kuendelea na safari ambapo tulilazimika kusimama na kuongeza majani ya chai na maji kila baada ya Kilometa 20 ili kupoza Injini ya gari iliyokuwa ikipata joto kutokana na kupasuka kwa rejeta. Na hiyo ndiyo iliyokuwa sababu kubwa ya kuchelewa kufika kwa “Babu”; tofauti na matarajio yetu.
Akitumia uzoefu wa kusafirisha watalii katika barabara za hifadhi za Taifa, dereva aliyekuwa akituendesha alitumia "ushujaa" mkubwa kuhakikisha kuwa tunafanikiwa kufika kijijini hapo pamoja na kuharibikiwa gari.
Sehemu kubwa ya barabara ya kwenda katika kijiji hicho ni mbovu sana na iliyojaa mashimo na vumbi jingi. Njiani tulikuta magari mengi yakiwa yameharibika na kushindwa kuendelea na safari ya kwenda Samunge.
2 comments:
Twashukuru sana mkuu kutupa ndogondogo ya `tukio la mwezi' maana hata wale waliokuwa hawajui kutamka jina la sehemu hiyo sasa wanalijua vyema-LOLIONDO.
Je ushuhuda gani wa kupona kwa mtu?
Au ndio siri ya jandoni haitolewi nje!
Wote ukiumwa unaomba upone, na hata ukiambiwa unywe mkojo utakuwanywa, lakini je wangapi wamepona na dawa hiyo toka kwa babu?
Huyu keshakua milionea magari yote hayo na umati huo.
Post a Comment