Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, March 10, 2011

Serikari yaagiza kusitisha tiba ya Loliondo kwa Babu Mchungaji Ambilikile Mwasapile

Babu akiongea na wananchi

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Shirima kuzuia haraka matibabu ya magonjwa sugu yanayoendeshwa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la KKKT, Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa Sale, Loliondo.

Dk Mponda alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzindua matumizi ya Bajaji kwa ajili ya kusafirishia wagonjwa. Alisema amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumzuia mchungaji huyo kuendelea na utoaji wa dawa mpaka serikali itakapojiridhisha na hali ya usalama pamoja na uwezo wa dawa hiyo.
“Kutokana na hali halisi ya usalama wa kiafya kwa sasa katika eneo hilo, kuna hatari ya kuwepo kwa milipuko ya magonjwa kwa kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka,” alisema Dk Mponda.
Hata hivyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Raymund Mushi alisema hajapata taarifa yoyote kuhusiana na hatua hiyo ya Wizara ya Afya... "Hadi jioni hii mpaka ninatoka ofisini sijapata taarifa yoyote kuhusiana na uamuzi huo."
Baadhi ya wananchi waliohojiwa kuhusiana na hatua hiyo ya Serikali walisema badala ya kuchukua hatua hiyo, ilipaswa kusimamia mchakato mzima wa utoaji wa dawa hiyo kwa kuhakikisha kwamba inatolewa katika mazingira mazuri na kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinapatikana kijijini hapo ikiwa ni pamoja na kuwabana wamiliki wa magari kupunguza nauli na kukarabati barabara.

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Serikali itaingilia kati kutokana na nguvu za mwili wa binadamu kupata kupona kutokana na imani tu kwamba atapona, nao wataalamu wanaita imani hiyo ya kupona "PLACEBO EFFECT".

Bahati mbaya PLACEBO EFFECT haidumu kamwe mwilini na kama kuna vijidudu katika damu ya mtu, PLACEBO hayiondowi kamwe!