Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, March 10, 2011

BREAKINGNEWSzzzzzz MWAKALEBELA NA MKEWE WAISHINDA TENA TAKUKURU

Mwakalebela wa pili kulia  na Mkewe na wadau wengine wakitoka Mahakamani Baada ya kuachiwa huru

Aliyekuwa mshindi katika kura za maoni ndani ya CCM katika jimbo la Iringa mjini kupitia CCM Frederick Mwakalebela na mkewe Celina leo wameachiwa na mahakama ya hakimu makzi Iringa katika kesi yao ya rushwa katika mchakato wa kura za maoni baada ya mahakama hiyo 

kuwaachia huru kuwa hawana kesi ya kujibu.

Leo mahakama hiyo ilikuwa ikitoa maamuzi madogo ya kuendelea ama kutoendelea katika kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru ) 
mkoa wa Iringa.

Hii ni mara ya pili sasa Mwakalebela kuishinda Takukuru mahakakani wiki iliyopita pia Mahakama pia ilimwachia Mwakalebela kabla ya Takukuru kumfungulia tena kesi Mwakalebela 
Hata hivyo wengi wamekuwa wakihoji sababu ya Takukuru Iringa kuendelea kung'ang'ania kesi hiyo huku watuhumiwa wengine wakiachiwa na mahakama bila kusumbuliwa kama Mwakalebela jambo ambalo wengi wanadai kuwa Takukuru ina jambo la siri katika kesi hiyo na si vinginevyo 

No comments: