Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, June 3, 2016

USAID YAJA NA MUAROBAINI WA HATI CHAFU KWENYE HALMASHAURI

Watumishi na watendaji wa Halmashauri ya Wanging'ombe wakiwa pamoja na wawezeshaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anatory Choya.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anatory Choya akizindua mradi wa Uimarishaji Mfumo wa Sekta za Umma unaofadhiliwa na USAID/TANZANIA

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anatory Choya akiteta jambo na Kiongozi wa timu ya uzinduzi Dkt Peter Kilima nje ya ukumbi wa Kyando mkoani Njombe

Kiongozi wa timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima akitoa taarifa za uzinduzi wa mradi Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma.

Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Rasilimali watu Ofisi ya Rais TAMISEMI Miriam Mmbaga akifafanua jambo wakati wa Uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya Sekta za Umma.


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anatory Choya akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Makete Daudi Yassin wakati wa uzinduzi wa uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma



SHIRIKA la msaada la Marekani USAID limekuja na muarobaini utakaoweza kuzisaidia Halmashauri za miji, Manispaa na Majiji kuepukana na hati chafu kwa kuanzisha mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya Sekta za Umma PS3.
Mradi huo wa wenye gharama ya Dola milioni 62 utaanza  kutekelezwa kwenye halmashauri 93  za miko 13 ya Njombe,Iringa,Morogoro,Mbeya,Lindi,Mtwara, Rukwa, Dodoma,Kigoma,Kagera, Mwanza,Shinyanga na Mara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo mkoani Njombe Kiongozi wa timu ya Uzinduzi wa mradi huo Dkt. Peter Kilima alisema kuwa mradi huo utazisaidia Halmashauri kujenga dhana shirikishi katika uimarisha mifumo ya sekta za utendaji kwa umma.
Alisema mradi huo wa miaka mitano umeanza Julai 2015 ambao utaendelea hadi Julai 2020 ambapo matarajio kila halmashauri katika halmashauri 93 zitafikiwa na mradi huo.
Dkt. Kilima alisema mifumo ya utekelezaji ipo katika sehemu 5 za Rasilimali watu,Rasilimali fedha,Mfumo wa TEHAMA na Tafiti Tendaji ambapo kwa sasa imeshazinduliwa katika mikoa 7 ya Iringa,Shinyanga,Dodoma,Mwanza,Mbeya, Mtwara na Rukwa.
Alisema mradi huo umbao umeandaliwa kwa kushirikiana na serikali ya Marekani na Tanzania unatekelezwa na mashirika saba yakiwemo ya Kitaifa na Kimataifa ambayo ni Abt Associates Inc ambaye ndiye mtekelezaji mkuu pamoja na watekelezaji wasaidizi.
‘’Mradi huo utaimarisha mfumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri, utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa’’alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Rasilimali watu,Ofisi ya Rais TAMISEMI, Miriam Mmbaga alisema mradi huu utatoa msaada wa kitaaluma katika ,kuimarisha mifumo iliyopo kwenye utawala wenye lengo la ushirikishwaji katika kuboresha utoaji huduma kwa jamii.
‘’Zipo changamoto zinazofahamika kwa watendaji,ushirikishwaji kwa watumishi wa halmashauri utasaidia kuboresha mahusiano’’alisema Mmbaga.
Awali Kaimu Mkuu wa mkoa wa Njombe Anatory Choya alisema wadau wa Halmashauri za wilaya wanapaswa kutumia vyema fursa hiyo kwa kuwa mradi huo ni muhimu kwa maendeleo ya mkoa na wilaya kwa ujumla.
Uzinduzi wa mradi huo umefanyika mkoani Njombe kwa kuwahusisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi,wenyeviti wa halmashauri na wakuu wa idara wapatao 170 wa mkoa huo.

No comments: