Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, June 28, 2016

SERIKALI YATAKIWA KUKAMILISHA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SONGWE.

 
Meneja wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani Mbeya, Hamis Amir akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari kutoka TAJATI (hawapo pichani).

Meneja wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani Mbeya, Hamis Amir akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari kutoka TAJATI.

Meneja wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani Mbeya, Hamis Amir akiwatembeza Waandishi wa habari kutoka TAJATI.

Meneja wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani Mbeya, Hamis Amir akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari kutoka TAJATI

Jengo la abiria ambalo halijakamilika.

Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda, Issa Hamad akitoa maelezo kwa Wana TAJATI.

Muonekano wa majengo katika uwanja wa ndege Songwe

Muonekano wa Uwanja wa ndege wa Songwe.

Senior Breafing officer wa Songwe airport akifafanua jambo

Muongoza ndege Bertila Ngowi akitoa maelezo na changamoto zinazowakabili. 
 
ILI kuongeza idadi ya Wawekezaji na Watalii kwa Mikoa ya Nyanda za Juu kusini, Serikali imetakiwa kukamilisha mara moja ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani hapa.
 
Imeelezwa kuwa ikiwa uwanja huo ukimaliziwa idadi kubwa ya Watalii na ndege kubwa zitaweza kutua na kuongeza  wawekezaji na kutoa fursa za kiuchumi kwa wakazi wa mikoa ya nyanda za juu.
 
Wito huo ulitolewa na Kaimu Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Hamisi Amiri,alipokuwa akizungumza na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji nchini(TAJATI)katika mwendelezo wa ziara zake nchini kuibua fursa za utalii na uwekezaji.
 
Amiri alisema hivi sasa uwanja huo unakabiliwa na Changamoto ya Jengo la kufikia abiria ambalo ujenzi wake umekwama kwa muda wa mwaka mmoja sasa kutokana na ukosefu wa fedha.
 
“jengo la kufikia abiria limekwama kuendelea na ujenzi kwa zaidi ya mwaka mmoja hivi sasa kutokana na serikali kukosa fedha za kumlipa mkandarasi zaidi ya shilingi bilioni kumi na moja kazi ambayo ingemalizika kwa kipindi cha miezi sita kama pesa zingekuwepo”alisema Meneja huyo.
 
Alisema  Serikali imetoa pesa kwa ajili ya ufungwaji wa taa katika njia ya kurukia ndege hivyo kuondoa adha ambayo wanakumbana nayo marubani wakati wa kutua na kuruka pindi kunapotokea hali ya mawingu katika uwanja huo ambao upo kwenye ukanda wa bonde la ufa.
 
Kwa upande wake Afisa usafirishaji wa abiria katika uwanja huo Jordan Mchami alisema kukamilika kwa jengo la abiria kutasaidia kuongezeka kwa mashirika mengine ya ndege ya kimataifa na kuongezeka kwa abiria na kwamba jengo hilo linaweza kupokea abiria zaidi ya elfu moja kwa wakati mmoja.
 
Baadhi ya waongozaji wa Ndege katika uwanja huo walisema  changamoto kubwa inayo wakabili katika uwanja huo ni pamoja na marubani kukumbana na  hali ya ukungu na ukosefu wa taa katika barabara ya kurukia ndege ambapo mara kadhaa ndege zimekuwa zikishindwa kutua kwa wakati na  pengine kurudi zilikotoka kutokana na hali hiyo.
 
Katika hitimisho la ziara hiyo Meneja wa Uwanja wa Ndege Amiri Hamisi alisema  waandishi wa Habari wana nafasi kubwa katika mchango wa uchumi kama ambavyo wameweza kuokoa uwanja mdogo wa zamani uliopo Kata ya Iyela uliokuwa umevamiwa na baadhi ya viwanja kuuzwa na baadhi ya wananchi kwa kushirikiana na mamlaka za umma.
 
Amiri alisema Waandishi baada ya kuitoa habari hiyo Serikali imetoa shilingi milioni mia sita(600,000/=) kwa ajili ya upimaji na umiliki kisheria ili kuzuia uvamizi ikiwa ni pamoja na kuweka uzio kwa ajili ya usalama ili kuzuia mifugo na watu wanaokatiza uwanjani pindi ndege zinapotua na kuruka katika uwanja wa ndege wa Songwe.
 
Ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Ulimboka Mwakilili ilitembelea huduma mbalimbali katika uwanja huo kama Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa,Kikosi cha Zimamoto na uokoaji,Uongozaji wa Ndege na Huduma za usafirishaji wa abiria.
 
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka wa Hali ya Hewa,Kanya ya Nyanda za juu kusini, Issah Hamadi alisema Idara hiyo ina vituo mbalimbali vya utabiri wa hali ya hewa ambavyo husaidia katika shughuli za anga na Kilimo na kwamba kituo hicho kilianzishwa mwaka 1929.
 
Issah alisema kituo hicho ambacho hufanya shughuli zake uwanja wa ndege wa zamani na Songwe kimepata tuzo ulimwenguni kutokana na huduma bora za utabiri wa hali ya hewa hivyo kuleta heshima kwa Taifa kutokana na utendaji wake bora.

No comments: