Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 30, 2016

YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE USAFIRI WA MAJI NA RELI

Mkuu wa Bandari ya Itungi Wilayani Kyela, Percival Salama akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari kwa Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) walipofanya ziara bandarini hapo.


Mkuu wa Bandari ya Itungi Wilayani Kyela, Percival Salama akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari kwa Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) walipofanya ziara bandarini hapo.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) Ulimboka Mwakilili akitoa historia ya uanzishwaji wa Chama hicho kwa Watumishi wa Bandari ya Itungi.




Watumishi wa Bandari pamoja na WanaTAJATI wakisikiliza kwa makini taarifa inayotolewa na Mkuu wa Bandari.
 
ILI kuondokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara unaotokana na usafirishaji wa mizigo mizito kwa umbali mrefu na kupelekea gharama kubwa kutumika katika ukarabati, Serikali imetakiwa kuwekeza zaidi kwenye njia ya Maji na Reli.
 
Wito huo ulitolewa  na Mkuu wa Bandari ya Itungi iliyopo Kyela Mkoani Mbeya,Percival Salama, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) waliofanya ziara bandarini hapo.
 
Salama alisema Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kukarabati na kutengeneza miundombinu ya barabara ambayo huharibika kutokana na usafirishaji wa mizigo mizito jambo ambalo huingizia hasara taifa.
 
Alisema ili kukabiliana na changamoto ya miundombinu ya barabara ni vema Serikali ikajikita katika kuboresha miundombinu ya Reli na usafiri wa majini kwa kuwa ndiyo unaweza kusafirisha mizigo mikubwa zaidi bila kuharibu miundombinu.
 
Alisema pia usafiri wa Reli na Maji ni rahisi hata kwa mfanyabiashara anayesafirisha biashara zake kutokana na mzunguko wake kuwa mfupi tofauti na matumizi ya barabara ambazo mara nyingi umbali wake ni mrefu.
 
Meneja huyo alitolea Mfano usafirishaji wa makaa yam awe kutoka Mbinga mkoani Ruvuma hadi Kiwanda cha Saruji cha Mbeya kilichopo Songwe kuwa husafiri kwa Kilomita 520 lakini endapo wangesafirishia Meli wangekuwa wanasafiri kilomita 420 tu hivyo kuokoa hata muda.
 
“Serikali ingetakiwa kujenga Reli kutoka Uyole hadi Kyela Itungi Port ambayo urefu wake hauzidi Kilomita 100 ambapo mizigo mingi inaweza kusafirishwa hadi ziwani kasha huingia kwenye meli hivyo kuondoa uharibifu wa miundombinu ya barabara na gharama kuwa nafuu” alisema Salama.
 
Aliongeza  kuwa ujenzi wa Reli kutoka Uyole jijini Mbeya hadi bandari ya Itungi Kyela ukiunganishwa na Reli ya Tazara utasaidia kurahisisha usafirishaji wa mizigo mikubwa kupitia Meli na Reli baada ya kukamilika kwa Meli kubwa za Mizigo zinazojengwa katika Bandari ya Itungi.
 
Alisema Meli zinazojengwa hapo zinatarajia kukamilika mwezi Agosti na Oktoba mwaka huu ambazo zitakuwa na uwezo wa kubeba na kusafirisha mizigo ya Tani 566.166 kila moja kwa wakati mmoja.
 
Aliongeza kuwa ilikuwa ni vema baada ya mizigo kushushwa katika bandari ya Itungi kutoka upande mwingine wa Ziwa ikabebwa kwa Reli na kuwapelekea wahusika na sio kusafirisha kwa barabara ili kutoziharibu kwa matumizi mengine.
 
Meneja Salama alisema kukamilika kwa ujenzi wa Meli hizo zinazojengwa na Mkandarasi mzawa kutoka Kampuni ya Songolo Marine transport Botyard  utatoa fursa kwa makampuni kusafirisha bidhaa zao  pamoja na malighafi kiurahisi.
 
Alisema hivi sasa kuna upungufu mkubwa wa usafirishaji wa mizigo katika bandari ya Itungi hali iliyotokana na kuharibika kwa Meli na kwamba mwaka 2011/2012 makaa yam awe pekee yalisafirishwa tani 26000 huku matarajio yakiwa ni tani 66000.

No comments: