Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, April 19, 2016

WANANCHI WAMETAKIWA KUJITOKEZA KUPATA DAWA ZA KINGA TIBA YA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Dk. Upendo Mwingira akifafanua jambo katika semina ya waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya kuhusiana na magonjwa hayo.

Afisa Programu ya Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Alistidia Simai akitoa mada katika Semina ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya kuhusiana na magonjwa hayo Semina iliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya hivi karibuni.

Mratibu wa Huduma za Elimu ya afya kwa umma kutoka Wizara ya afya, Said Makora akifanunua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) katika semina kuhusu magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyofanyika hivi karibuni mkoani MbeyaBaadhi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya wakifuatilia Semina kuhusu Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

IMEELEZWA kuwa chanzo cha kuongezeka kwa  magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele kimetokana na imani potofu na umaskini miongoni mwa jamii hali iliyopelekea kushindwa kupata matibabu kwa wakati.
 
Hayo yalibainishwa  na Mratibu wa Magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele wa Wizara ya Afya, jinsia, maendeleo ya jamii, wazee na watoto, Dk. Upendo Mwingira wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya na Songwe yaliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
 
Dk. Mwingira alisema jamii nyingi iliyachukulia magonjwa hayo kama suala la kiimani na kwamba haikujua kama matibabu yapo na mgonjwa huweza kupona kabisa ambapo pia elimu ndogo na umaskini unachangia kutotambua namna ya kukabiliana nayo.
 
Aliyataja magonjwa hayo kuwa ni Usubi unaosababishwa na minyoo inayoenezwa na inzi weusi, Matende na Mabusha yanayoenezwa na mbu aina ya culex na Anopheles, Trakoma inayosababishwa na bacteria,Kichocho kinachosababishwa na konokono pamoja na ugonjwa wa minyoo ya tumbo.
 
Alisema magonjwa hayo yanapatikana zaidi katika mikoa ya ukanda wa Pwani ambapo utafiti umeonesha kuyakumba maeneo mengine ya Nchi ambapo alisema magonjwa mengine ni Malale, Kichaa cha Mbwa,Tegu, Bruceloza na ugonjwa wa Tauni.
 
Aliongeza kuwa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha inahamasisha jamii ya Watanzania walioathirika na magonjwa hayo pamoja na wengine wanatumia dawa za kinga tiba bila kujali kama amepata maambukizi au hajapata ili baadhi ya magonjwa kuyadhibiti na mengine kuyatokomeza kabisa hadi ifikapo 2020.
 
Alisema zoezi la kugawa daza za kingatiba limeshaanza kwa baadhi ya mikoa ambapo asilimia kubwa ya dozi ni mwaka mmoja na kwamba dawa hizo zitatolewa bure kwa kila mwananchi kupitia kila kaya au vituo vya afya na zahanati.
 
Akizungumzia malengo ya mafunzo hayo kwa waandishi wa habari, Dk. Mwingira alisema ni kufikisha ujumbe kwa jamii kwa haraka juu ya magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele ili wananchi wapate elimu na kutumia dawa za kinga tiba.
 
Aliongeza kuwa lengo linguine ni kuwawezesha wanahabari kuelewa undani juu ya mpango wa kudhibiti na kuyatokomeza magonjwa hayo, kuwawezesha kutoa elimu kwa jamii na kuwajengea uwezo na uelewa kwa jamii kuhusiana na faida ya dawa zenye kingatiba.

No comments: