Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Nyerembe Munasa Sabi akiongea na waandishi wa habari(Hawapo pichani) kuhus harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari Iyunga yaliyoteketea kwa moto hivi karibuni kulia ni Kaimu Mkurugenzi Jiji la Mbeya Bw.Dkt Samwel Lazaro.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Nyerembe Munasa Sabi akiongea na waandishi wa habari(Hawapo pichani) kuhus harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari Iyunga yaliyoteketea kwa moto hivi karibuni kulia ni Charles Mwakipesile Mdau wa Maendeleo na kushoto ni Afisa Habari Idara ya Habari Raymond Mushumbusi.
Picha zote na Beatrice Lyimo MAELEZO
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Waziri
Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee
itakafanyika kesho katika ukumbi wa Ubungo Plaza kwa ajili ya kuchangia
fedha zitakazowezesha kukarabati mabweni manne ya shule ya Sekondari ya
Ufundi ya Iyunga yaliyoungua hivi karibuni.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Wilaya ya Mbeya
Mhe. Nyerembe Munasa Sabi amesema kuwa wameamua kuomba nguvu kutoka kwa
wadau wa elimu na watanzania kwa ujumla kujumuika katika kuchangia
shule ya sekondari ya ufundi Iyunga ili waweze kukarabati mabweni
yaliyoungua kwa moto.
“ Hadi
sasa takribani wanafunzi 421 hawana mahala pa kulala kutokana na
kuteketea kwa mabweni na kwa kushirikiana na TAMISEMI tumeamua kusitiza
masomo kuanzia tarehe11 March hadi tarehe 01 Aprili ili kupisha
ukarabati wa mabweni”
“
Tumeanza ujenzi wa baadhi ya miundombinu iliyoteketea na mabweni ikiwa
ni jitihada za wadau mbalimbali waliochangia kutoka Mbeya na nawasihi
wanambeya wale waliosoma shule ya Iyunga na shule za Mbeya na watanzania
kwa ujumka kujitokeza kesho katika harambee hii” Alisema
Mhe.
Nyerembe Munasa Sabi aneongeza kuwa wamepokea michango mbalimbli kutoka
kwa wadau wakiwemo Mbeya Cement waliotoa mifuko 1,000 ya saruji kwa
ajili ya ujenzi na kwa sasa mahitaji yaliyopo ni takribani Shillingi
million 770 ili kukarabati na kujenga majengo mapya kwa ajili ya shule
hiyo.
Shule ya Sekondari ya Ufundi
Iyunga yenye wanafunzi takribani 9970 kuanzia kidato cha kwanza hadi
cha sita imekumbwa na majanga ya moto ambayo yamesababisha athari kwa watoto
kutoendelea na masomo na uharibifu wa miundombinu ila Serikali kupitia
TAMISEMI na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wamejipanga kukusanya fedha kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa shule hiyo.
No comments:
Post a Comment