Naibu mkurugenzi wa huduma kwa watumiaji bidhaa za mawasiliano wa Thadayo
Ringo akionesha simu feki inavyofanana na simu halali.
Mhandisi mfumo Rajisi Imelda Salum akifundisha namna ya kutofautisha simu feki
Eng: Lilian Mwangoka akifafanua jambo kwa waandishi
Baadhi ya waandishi wakisikiliza kwa makini maelezo ya viongozi wa mamlaka ya mawasiliano TCRA
Mwandishi wa gazeti la Uhuru Solomoni Mwansele akitazama kwa makini kuibaini simu feki
Katibu Mkuu wa Chama cha waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania TAJATI Venance Matinya akiuliza swali
Mwandishi wa habari gazeti la Majira Rashidi Mkwinda akiuliza swali
Mwandishi wa habari Star Tv Amina Saidi akiomba ufafanuzi
Mwandishi wa Habari gazeti la Mwananchi Brand Nelson akiomba mwongozo wa jambo fulani
Naibu katibu Mkuu TAJATI Patrick Kosima akiuliza swali.

ILI kudhibiti vifaa vya
mawasiliano visivyokuwa na ubora kwa mtumiaji, Wananchi wametakiwa kujenga
utamaduni wa kudai risiti pindi anaponunua na kuhakikisha muuzaji anatoa muda
wa garantii usiopungua miezi kumi na mbili kwa kifaa alichouza.
Wito huo ulitolewa jana na
Naibu Mkurugenzi wa huduma za mawasiliano kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano,(TCRA)Thadayo Ringo,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani
nchini(CEIR) katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za TCRA Kanda ya
Nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
Ringo alisema Mamlaka hiyo
imejipanga kuanza kuzima simu za kiganjani ambazo ni feki usiku wa saa sita
mwezi Juni mwaka huu hivyo ili kuepuka na kuzimiwa Simu ni vema wateja wakawa
na utaratibu wa kudai risiti na kupewa muda wa garantii ili ikizimwa iwe rahisi
kuirudisha kwa muuzaji.
Alisema mbali na mteja kudai
risiti na kupewa muda wa garantii usiopungua miezi 12 utamsaidia mwananchi kurudisha
simu au kifaa cha mawasiliano endapo kitakuwa kimeharibika kabala ya muda huo nay
eye kutengenezewa ama kubadilishiwa bidhaa nyingine.
Aliongeza kuwa kupitia mfumo
huo utairahisishia mamlaka kumbaini muingizaji wa bidhaa zisizokuwa na ubora
kutokana na kufuatilia mlolongo mzima wa muuzaji hadi kumpata mwagizaji ili
aweze kudhibitiwa kwa mujibu wa sheria.
Mkurugenzi huyo alisema kupitia
mfumo wa rajisi ambao utakuwa na njia tatu ambazo ni orodha ya namba tambulishi
ambazo vifaa vyake vinaruhusiwa, orodha ya namba tambulishi ambazo
hutolewa kuwa zimefungiwa na namba
tambulishi ambazo zimefungiwa kwa muda au kuruhusiwa kwa muda utasaidia
kurahisisha huduma za mawasiliano.
Alizitaja faida za mfumo wa
rajisi ya namba tambulishi kuwa utasaidia kudhibiti wizi wa simu ambapo mtu
aliyeibiwa ama kupoteza simu anaweza kutoa taarifa kwenye mamlaka na kasha kuifunga
ili isifanye kazi tena.
Alisema faida nyingine ya mfumo
huo utasaidia kuhimiza utii wa sheria kwa mujibu wa kifungu cha 128 cha EPOCA
ambacho kinamtaka mtumiaji wa simu kutoa taarifa ya kupotea kwa simu au laini
sambamba na kampuni ya simu kutokutoa huduma kwa simu iliyofungiwa.
Alisema faida nyinine ni
kujenga misingi ya matumizi ya simu halisi zisizo bandia ambapo mtumiaji ataweza
kutambua iwapo simu aliyonayo inakidhi viwango na ni halisi sio bandia kwa
kubonyeza alama zilizowekwa na mamlaka.
“Mmiliki wa simu anapiga nyota
reli sifuri sita kasha reli anapata
namba zake za utambulisho yaani Imei ambazo anazituma kwenda 15090 hapo
analetewa maelezo kuwa simu anayotumia inaoana kati ya kampuni iliyotengeneza
na imei namba” alifafanua Naibu Mkurugenzi.
No comments:
Post a Comment