|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala
akizungumza na watumishi waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi na
Mkuu wa Mkoa mstaafu Abbas Kandoro Machi 17 mwaka huu.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mstaafu Abasi
Kandoro (kulia) akimkabidhi rasmi ofisi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala
katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Machi 17
mwaka huu.
|
Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abas Kandoro
akizungumza na watumishi na baadhi ya viongozi (hawapo pichani)waliohudhuria
hafla ya makabidhiano ya ofsini na Mkuu wa Mkoa mpya Amosi Makala Machi 17
mwaka huu.
|
|
|
Watumishi wa Serikali wakisikiliza kwa makini maagizo ya
Mkuu wa Mkoa huo Amos Makala wakati
akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abasi
Kandoro Machi 17 mwaka huu
|
|
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja akimkabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya kumaliza makabidhiano ya ofisi na Mstaafu Abbas Kandoro |
WATUMISHI wa Mkoa wa Mbeya wametakiwa kuacha kufanya kazi
kwa mazoea bali kila mtu anapaswa kuwajibika kwa kufanya kazi kwa ushirikiano
ili kuwaletea tija wananchi kwenye maeneo yao.
Rai hiyo ilitolewa na
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipokuwa akizungumza na baadhi ya
Watumishi wa Mkoa wa Mbeya waliojitokeza katika hafla ya makabidhiano ya Ofisi
baina yake na Mkuu wa Mkoa aliyestaafu Abbas Kandoro.
Makalla alisema kila mtumishi akiwajibika katika eneo lake
litachangia kuondoa ombwe katika uongozi ambapo kila mwananchi atapata huduma
katika ngazi husika ili kuondoa maandamano ya wananchi kudai haki na kutaka
kero zao zitatuliwe na Mkuu wa Mkoa.
“Nimekuja hapa kwa lengo la kukumbushana sina jipya kinachotakiwa
ni uwajibikaji, tuwatumikie wananchi wetu, haiwezekani suala dogo mtu anafunga
safari kwenda kwa Mkuu wa Mkoa nataka masuala ya Mkuu wa Mkoa yawe na hadhi ya
Mkuu wa Mkoa” alifafanua Makalla.
Alisema ili kuepusha kukaa na matatizo ya wananchi pamoja na
migogoro inayoweza kutatulika ni lazima kila Mkuu wa Wilaya pamoja na wataalam
wake kutenga siku moja ya kukaa ukumbini kusikiliza shida mbali mbali za
wananchi ili zinazoshindikana anapeleka mbele.
“Naagiza kila alhamisi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane
mchana Mkuu wa Wilaya pamoja na wataalam wako mtakaa ukumbini ili kusikiliza na
kujibia shida za wananchi kabla taarifa haijafika kwangu” alisema Mkuu wa Mkoa.
Aliongeza kuwa Watumishi wanaojihusisha na mitandao ya
kijamii muda wa kazi wanapaswa kujirekebisha kwani hatakuwa mvulimivu kwa mtu
yoyote ambaye atashindwa kutimiza wajibu wake kwa jamii.
Mbali na hayo Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza watumishi wote
kuhakikisha wanasimamia usafi wa mazingira ili ugonjwa wa kipindupindu
usijirudie au kuwepo katika Mkoa wa Mbeya.
Awali akikabidhi taarifa ya Mkoa wa Mbeya kwa Mkuu wa
Mkoa Amos Makalla, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya aliyemaliza muda wake, Abbas
Kandoro alisema anawashukuru marais wa awamu zote kwa kumuamini na kumpa
majukumu kwa kipindi chote cha uongozi wake.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru Marais wa awamu
zote kuanzia awam ya kwanza ya Mwalimu Nyerere kwani nilianza kazi serikalini
mwaka 1976 hadi leo ambapo Dk. Magufuli aliniona katika kipindi cha miezi
mitano ambapo hadi leo nimefikisha miaka 40 ya utumishi sio haba” alisema
Kandoro.
Aidha alisema amefanya kazi yenye mafanikio katika Mkoa wa
Mbeya kutokana na ushirikiano alioupata kutoka kwa watumishi kuanzia ngazi ya
chini hadi kamati ya ulinzi na usalama za Wilaya ya Mkoa.
“Niseme tu kuwa wanaoishi Mkoa wa Mbeya ni watu wenye
misimamo ambao ukienda bila utaratibu hawasikii lakini ukiwatumia na
kuwashirikisha watumishi wengine hadi ngazi ya chini mambo mengi yanafanikiwa”
alifafanua Kandoro.
Hata hivyo Kandoro alivipongeza vyombo mbali mbali vya
habari kuwa vimekuwa daraja muhimu la kuwaunganisha watumishi na wananchi
katika maeneo mbali mbali hivyo kumuomba Mkuu wa Mkoa kuimarisha daraja hilo
ili lisibomoke.
No comments:
Post a Comment