Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa katika kikao wakijadili namna wananchi wanavyoweza kunufaika na Uatalii wakati wa Kupatwa kwa jua. |
WAKAZI
wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wametakiwa kujiandaa kupokea wageni kutoka
ndani na nje ya Nchi kwa kuweka vitega uchumi mbali mbali vitakavyoweza
kuwavutia watalii kwa kuweza kuinua vipato vyao.
Rai
hiyo imetolewa kutokana na kuwepo kwa taarifa ya kutokea kwa tukio kubwa la
kihistoria nchini ambapo Septemba mosi mwaka huu Wilaya ya Mbarali itaingia
kwenye historia ya kisayansi duniani na dunia kuhamia hapo katika tukio kubwa
la kupatwa kwa jua litakalotekea majira ya saa moja na nusu asubuhi siku hiyo.
Tukio
hilo la kipekee duniani, linatarajiwa kuvutia wataalamu wa masuala ya unajimu
kutoka sehemu mbali mbali duniani na watalii wa nje na ndani ya nchi
ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakifuatilia mzunguko wa mwezi na dunia.
Uchunguzi
uliofanywa na Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI)
umebaini kuwa baadhi ya makampuni ya utalii ya nje na ndani yameanza
maandalizi kwa ajili ya tukio hilo la kipekee, ambapo idadi kubwa ya
watalii wa nje wanatarajia kuwepo mkoani Mbeya kushuhudia tukio hilo pamoja na
kufurahia vivutio vingine vya utalii vilivyopo nchini.
Akizungumza
wakati akichangia kwenye kikao cha Kamati ya Utalii Mkoa wa Mbeya, kilichokuwa
na kazi ya kupitia mpango mkakati wa miaka mitano wa kukuza utalii katika Mikoa
ya Kanda ya kusini,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusafirisha watalii ya UPL
Safaris & Tour, Gabriel Shawa alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo kamati
hiyo.
Shawa
aliwaeleza waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji jijini Mbeya, jana,
kuwa baada ya kubaini kuwepo kwa tukio hilo la kihistoria na nadra
kutokea na kuonekana kwa uzuri zaidi kusini mwa Afrika mkoani Mbeya, wao kama
watoa huduma za utalii mkoani humo tayari wameanza maandalizi ya malazi
kwa wageni wao na kuyatambua maeneo ya vivutio kwa ajili ya watalii hao.
Hata
hivyo, pamoja na kuwepo kwa tukio hilo na maandalizi yake, ilibainika kuwa sio
wenye hoteli wala viongozi wa serikali au wasimamizi wa sekta hiyo ya utalii
waliokuwa wanaufahamu wa kuwepo kwa tukio hilo na maandalizi ya kuwapokea
wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Kwa
mujibu wa maelezo ya kisayansi kuhusu tukio hilo, kupatwa kwa jua hutokea pale
mwezi unapopita kati ya dunia na jua hivyo kuzuia mwanga wa jua kuifikia dunia
au kuifikia kwa kiwango cha mwanga hafifu.
Mtandao
wa http://eclipse.astronomie.info/sofi unaonyesha
kwamba tukio la kupatwa kwa jua mkoani Mbeya na hususani katika wilaya ya
Mbarali litaonekana majira ya asubuhi na wananchi wataweza kulishudia
tukio hilo kwa kutumia vifaa maalumu ya kuonea kupatwa kwa jua.
Kanda
ya Kusini ipo katika mkakati mkubwa wa kuendeleza utalii katika mikoa yake
ambayo huko nyuma haikupewa nafasi ya kuwa sehemu nzuri ya utalii, japokuwa ni
ukanda wenye vivutio vingi na vya aina anuai.
Katika
kuviendeleza vivutio hivyo Mkoa wa Mbeya umeandaa Mpango Mkakati wa kukuza na
kuendeleza utalii mkoani humo ambao utawezesha kutangaza, kukuza na kuendeleza
sekta ya utalii mkoani humo nakuongeza pato la jamii na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti
wa TAJATI,Ulimboka Mwakilili alisema kuwa timu ya waandishi hao wanaendelea
kufuatilia habari za tukio hilo na kuzidi kutangaza vivutio vya utalii ili
kuweza kuwavutia watalii wengi wa ndani na nje wakisukumwa na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment