Mkurugenzi wa VETA kanda ya Kusini Magharibi, Justin Rutta akizungumza katika mahafali ya wahitimu walipata mafunzo katika mfumo usiorasmi(RPL) yaliyofanyika jijini Mbeya. |
Kaimu Mkurugenzi wa VETA nchini Geophrey Sabuni akizungumza katika Mahafari ya wahitimu waliopata mafunzo ya ufundi katika mfumo usio rasmi Kanda ya kusini Magharibi. |
Mkuu wa Chuo cha VETA Kanda ya kusini Magharibi Lameck Kihinga akitoa taarifa ya hali ya Chuo na kozi zitolewazo na chuo hicho Kanda |
Mwenyekiti wa Wakufunzi wa Mafunzo yasiyopitia kwenye mfumo rasmi, Paul Kakaku akisalimiana na Wahitimu (hawapo pichani) |
Wahitimu wakikabidhiwa vyeti |
Baadhi ya Wakufunzi wakifuatilia sherhe za mahafali |
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali |
Wahitimu wakisoma Risala yao kwa mgeni rasmi |
Mhitimu Majaliwa Sandules akikabidhi Risala kwa mgeni rasmi |
Wahitimu na Wageni wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti |
MAFUNDI wa fani mbali mbali
wasiopitia katika mfumo rasmi wa mafunzo wamelalamikia vitendo vya baadhi ya
mafundi waliosoma kuwanyonya na kuwalipa ujira mdogo katika kazi zao kutokana
na kutokuwa na vyeti vya kuwatambua.
Hayo yalibainishwa na wahitimu wa Kozi isiyo rasmi ya Mafundi wa mitaani iliyotolewa na Chuo
cha Ufundi Stadi Veta Kanda ya Kusini Magharibi katika Mahafali ya kuwatunuku
vyeti na kuwaingiza katika mfumo rasmi.
Wakizungumza katika risala yao mbele
ya mgeni rasmi, Wahitimu hao walisema kabla ya kutambulika katika mfumo rasmi
walikuwa wakinyonywa na kulipwa ujira mdogo kutoka kwa wasimamizi wao kwa
kisingizio cha kusoma.
“Kinachotushangaza zaidi ni
kwamba wenzetu wenye vyeti ambao walipita katika mfumo rasmi wanatutumia zaidi
sisi katika kufanikisha kazi zao kwa malipo kidogo kiasi kwamba wao ndiyo
wanaonufaika zaidi kwa kazi za mikono yetu” ilisema Risala ya wahitimu
iliyosomwa na Majaliwa Sandules
Mafundi hao ambao waliingizwa
kwenye mfumo rasimi kutokana na fani zao za awali ambazo ni upishi, ufundi
seremala, ufundi uashi, ufundi wa magari pamoja na vyakula na vinywaji.
Walisema mbali na kuboreshewa
fani zao pia wamefundishwa ujasiliamali, mawasiliano ya kibiashara, huduma kwa
wateja,kujali ubora wa kazi, mahusiano na afya ya uzazi, usalama na afya mahala
pa kazi, ukarabati kinga na masomo ya fani.
Aidha walipongeza Veta kwa
kushirikiana na Shirika la Kazi duniani(ILO) kwa kuanzisha mfumo huo kwani
hakuna gharama walizochangia kuanzia mchakato wa kuwaainisha, kuwatambua,
kuwafanyia tathmini na hatimaye mafunzo.
Awali Mratibu wa Mafunzo
hayo,Eshiwakwe Lema alisema mafunzo yalianza Agosti Mwaka jana ambapo Mafundi
252 waliandikishwa kati yao 156 walifaulu na 13 walifeli huku 83 wakiwa
wamekacha kabisa.
Alisema waliofanikiwa kuhitimu
na kutunukiwa Vyeti ni 167 kati yake wanawake ni 21 na wanaume ni 146 na
kuongeza kuwa mafunzo hayo yalikabiliana na changamoto kubwa ya kisiasa kwani
mpango ulianza kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu hivyo wengi walidhani ni
sehemu ya kukipigia kampeni chama cha siasa.
Naye Mwenyekiti wa Wakufunzi,
Paul Kakaku alisema mfumo huo ulianza mwaka 2010katika Mikoa ya Lindi, Mtwara,
Morogoro, Mwanza na Dar es salaam ambako huko walikuwa wakifanya majaribio
lakini zoezi la kuanza kutoa vyeti limeanza rasmi Mbeya na kwamba hadi sasa ni
vijana 600 wamenufaika na mfumo huo.
Alisema mafunzohayo yanatolewa
na walimu kutoka VETA za Kanda ya Kusini Magharibi na Nyanda za juu kusini kwa
mikoa ya Iringa, Makete, Songea, Mbeya na Mpanda.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi
ambaye ni Mkurugenzi wa VETA kanda ya Kusini Magharibi, Justine Ruta
aliyefuatana na Mkurugenzi wa Mitihani makao makuu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Veta, Geophrey Sabun alisema wahitimu wanapaswa kujiendeleza zaidi na kutafuta
tenda kutoka Halmashauri mbali mbali kwa kubuni na kutengeneza thamani zenye
ubora.
No comments:
Post a Comment