Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, February 8, 2016

VETA KWA USHIRIKIANO NA ILO YAWATAMBUA MAFUNDI WASIOPITIA MFUMO RASMI


Mkurugenzi wa VETA kanda ya Kusini Magharibi, Justin Rutta akizungumza katika mahafali ya wahitimu walipata mafunzo katika mfumo usiorasmi(RPL) yaliyofanyika jijini Mbeya.


Kaimu Mkurugenzi wa VETA nchini Geophrey Sabuni akizungumza katika Mahafari ya wahitimu waliopata mafunzo ya ufundi katika mfumo usio rasmi Kanda ya kusini Magharibi.

Mkuu wa Chuo cha VETA Kanda ya kusini Magharibi Lameck Kihinga akitoa taarifa ya hali ya Chuo na kozi zitolewazo na chuo hicho Kanda

Mwenyekiti wa Wakufunzi wa Mafunzo yasiyopitia kwenye mfumo rasmi, Paul Kakaku akisalimiana na Wahitimu (hawapo pichani)


Wahitimu wakikabidhiwa vyeti


Baadhi ya Wakufunzi wakifuatilia sherhe za mahafali

Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali

Wahitimu wakisoma Risala yao kwa mgeni rasmi

Mhitimu Majaliwa Sandules akikabidhi Risala kwa mgeni rasmi

Wahitimu na Wageni wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti


MAFUNDI wa fani mbali mbali wasiopitia katika mfumo rasmi wa mafunzo wamelalamikia vitendo vya baadhi ya mafundi waliosoma kuwanyonya na kuwalipa ujira mdogo katika kazi zao kutokana na kutokuwa na vyeti vya kuwatambua.

Hayo yalibainishwa  na wahitimu wa Kozi isiyo rasmi ya Mafundi wa mitaani iliyotolewa na Chuo cha Ufundi Stadi Veta Kanda ya Kusini Magharibi katika Mahafali ya kuwatunuku vyeti na kuwaingiza katika mfumo rasmi.

Wakizungumza katika risala yao mbele ya mgeni rasmi, Wahitimu hao walisema kabla ya kutambulika katika mfumo rasmi walikuwa wakinyonywa na kulipwa ujira mdogo kutoka kwa wasimamizi wao kwa kisingizio cha kusoma.

“Kinachotushangaza zaidi ni kwamba wenzetu wenye vyeti ambao walipita katika mfumo rasmi wanatutumia zaidi sisi katika kufanikisha kazi zao kwa malipo kidogo kiasi kwamba wao ndiyo wanaonufaika zaidi kwa kazi za mikono yetu” ilisema Risala ya wahitimu iliyosomwa na Majaliwa Sandules

Mafundi hao ambao waliingizwa kwenye mfumo rasimi kutokana na fani zao za awali ambazo ni upishi, ufundi seremala, ufundi uashi, ufundi wa magari pamoja na vyakula na vinywaji.

Walisema mbali na kuboreshewa fani zao pia wamefundishwa ujasiliamali, mawasiliano ya kibiashara, huduma kwa wateja,kujali ubora wa kazi, mahusiano na afya ya uzazi, usalama na afya mahala pa kazi, ukarabati kinga na masomo ya fani.

Aidha walipongeza Veta kwa kushirikiana na Shirika la Kazi duniani(ILO) kwa kuanzisha mfumo huo kwani hakuna gharama walizochangia kuanzia mchakato wa kuwaainisha, kuwatambua, kuwafanyia tathmini na hatimaye mafunzo.

Awali Mratibu wa Mafunzo hayo,Eshiwakwe Lema alisema mafunzo yalianza Agosti Mwaka jana ambapo Mafundi 252 waliandikishwa kati yao 156 walifaulu na 13 walifeli huku 83 wakiwa wamekacha kabisa.

Alisema waliofanikiwa kuhitimu na kutunukiwa Vyeti ni 167 kati yake wanawake ni 21 na wanaume ni 146 na kuongeza kuwa mafunzo hayo yalikabiliana na changamoto kubwa ya kisiasa kwani mpango ulianza kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu hivyo wengi walidhani ni sehemu ya kukipigia kampeni chama cha siasa.

Naye Mwenyekiti wa Wakufunzi, Paul Kakaku alisema mfumo huo ulianza mwaka 2010katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro, Mwanza na Dar es salaam ambako huko walikuwa wakifanya majaribio lakini zoezi la kuanza kutoa vyeti limeanza rasmi Mbeya na kwamba hadi sasa ni vijana 600 wamenufaika na mfumo huo.

Alisema mafunzohayo yanatolewa na walimu kutoka VETA za Kanda ya Kusini Magharibi na Nyanda za juu kusini kwa mikoa ya Iringa, Makete, Songea, Mbeya na Mpanda.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa VETA kanda ya Kusini Magharibi, Justine Ruta aliyefuatana na Mkurugenzi wa Mitihani makao makuu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Geophrey Sabun alisema wahitimu wanapaswa kujiendeleza zaidi na kutafuta tenda kutoka Halmashauri mbali mbali kwa kubuni na kutengeneza thamani zenye ubora.


No comments: