MNYAMA ambaye huo anaonekana
kwa nadra maeneo mengi nchini na baada ya kuonekana hua na ujumbe pamoja na
utabiri katika jamii ameonekana kwa mara ya kwanza katika Hifadhi ya Taifa ya
Kitulo tangu kuanzishwa.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa Kitulo, Rimus Mkongwe alithibitisha kuonekana kwa mnyama huyo na kuongeza kuwa
alikutwa na askari wa Hifadhi walipokuwa wakifanya doria ndani ya hifadhi
ambapo walimuona maeneo ya Mwakipembwa katika uwanda wa Nyasi.
Alisema walishindwa kupata
ujumbe au utabiri wake kutokana na Askari hao kutokuwa na mahitaji muhimu
ambayo Mnyama huyo anapaswa kupewa ili atoe utabiri wake ama ujumbe anaokuwa
nao.
Alivitaja vitu hivyo kuwa ni
pamoja na Panga, Mkuki na Unga na kuongeza kuwa Mnyama huyo bado yuko ndani ya
hifadhi na atahifadhiwa kwa ajili ya watu wanaotaka kumuona hivyo kuongeza
kivutio ndani ya Hifadhi.
No comments:
Post a Comment