Madawa ya kulevya aina ya Bhangi yakiwa kwenye begi baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi |
Bhangi ikiwa imesindikwa tayari kwa kusafirishwa |
KATIKA
TUKIO LA KWANZA,
MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NURU
ISMAIL [31] MFANYABIASHARA NA MKAZI WA JIJINI DAR ES SALAAM ANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI UZITO KILO 7 NA GRAMU 100 ZIKIWA
ZIMEHIFADHIWA KWENYE MABEGI YA NGUO.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.01.2016 MAJIRA YA SAA 05:30 ASUBUHI HUKO CUSTOM MPAKANI
MWA TANZANIA NA ZAMBIA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA
MBEYA.
AIDHA MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA
SAFARINI AKITOKEA SOUTH AFRIKA KUELEKEA JIJINI DSM AKIWA NA PASSPORT NO. AB.767234 ILIYOTOLEWA DSM TAREHE 21/10/2015 NA KUSAFIRI KWENYE
BASI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.595 BPR
MALI YA KAMPUNI YA FALCON IKITOKEA LUSAKA KUELEKEA DSM.
KATIKA
TUKIO LA PILI,
MTU MMOJA MKAZI WA BITIMANYANGA WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA AITWAYE HAMIS SELEMANI [30] ANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 3 SAWA NA UZITO WA GRAMU 15 ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA MFUKONI MWA
SURUALI YAKE.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.01.2016 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KIJIJI CHA
BITIMANYANGA, KATA YA MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA.
WATUHUMIWA WATAFIKISHWA
MAHAKAMANI MARA TU BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
No comments:
Post a Comment