|
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Francis Namaumbo akifafanua jambo kwa Wanachama wa TAJATI (Hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha |
|
Makamu Mwenyekiti wa TAJATI Christopher Nyenyembe (wa kwanza kushoto) akifuatilia kwa makini majadiliano na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete na Wanatajati walipomtembelea ofisini kwake |
|
Msimamizi Msaidizi wa miradi ya kijamii wa WCS akifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea |
|
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete (mwenye suti ya kaki waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa TAJATI na baadhi ya watumishi wa WCS na Halmashauri. |
|
Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Kitulo akitoa maelezo kwa wanachama wa TAJATI walimpomtembelea ofisini kwake |
|
Wanachama wa TAJATI wakiwa ndani ya Hifadhi ya Kitulo |
|
Faraja Dembe msimamizi msaidizi wa Miradi ya kijamii kutoka WCS akionesha eneo ambalo limeondolewa mimea vamizi kupisha uoto wa asili |
|
Ua aina ya Chikanda linalopatikana Kitulo |
|
Mbunge wa Makete Dk. Norman Sigalla King akisalimiana na Mwanachama wa TAJATI baada ya kukutana katika Ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete |
|
Watumishi wa WCS wakiwaongoza wanachama wa TAJATI walipotembelea ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete |
|
Moja ya Maua aina 40 zinazopatikana katika hifadhi ya Kitulo pekee |
|
Aina ya Mimea Vamizi ndani ya Hifadhi ya Kitulo ikiwa imeshaangushwa tayari kuondolewa |
|
Wana TAJATI wakiwa kwenye moja ya magari yaliyotolewa na WCS kwa ajili ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Kitulo |
SHIRIKA la WCS lililochini ya
Mpango wa Shirika la msaada la Serikali ya watu wa Marekani(USAID) mwishoni mwa
wiki liliwawezesha waandishi wa habari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Kitulo.
Waandishi waliowezeshwa
kutembelea hifadhi ya Kitulo ni Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za
Utalii na Uwekezaji nchini Tanzania (TAJATI).
Katika ziara hiyo Wanatajati
walitembelea hifadhi ya Kitulo kwa lengo la kujitambulisha ikiwa ni siku chache
tangu kupata usajili na msajili wa vyama vya Kijamii chini ya Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka
Mwakilili alisema lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kujitambulisha pamoja na
kutembelea miradi inayoendeshwa na WCS ili kujionea changamoto na mafanikio
wanayokutana nayo.
Alisema mbali na kujionea
Shughuli za WCS pia walipata fursa ya kukutana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Makete ambaye alieleza fursa zinazoweza kupatikana ikiwa Wilaya hiyo
itatangazwa vizuri.
Kwa upande wao,WCS wakiongozwa
na Msimamizi msaidizi wa miradi ya kijamii, Faraja Dembe na Muikolojia Vicky
Felix walisema mradi unaoendelea ni uondoaji wa mimea vamizi katika Hifadhi ya
Kitulo.
Walisema mimea hiyo inachangia
kuondoa uoto wa asili na kukausha vyanzo vya maji ya Mto Ruaha na ziwa Nyasa.
Waliitija aina ya mimea
inayoondolewa kuwa ni pamoja na miti aina ya Cyprus, Pine, Black wattle na Eucalyptus
ambayo ilipandwa kwa lengo la kupunguza ardhi oevu katika makazi ya watu kabla
ya kuwa hifadhi.
No comments:
Post a Comment