Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, December 9, 2015

WILDLIFE CONSERVATION SOCIETY (WCS) YADHAMINI ZIARA YA TAJATI HIFADHI YA KITULO.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Francis Namaumbo akifafanua jambo kwa Wanachama wa TAJATI (Hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha

Makamu Mwenyekiti wa TAJATI Christopher Nyenyembe (wa kwanza kushoto) akifuatilia kwa makini majadiliano na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete na Wanatajati walipomtembelea ofisini kwake

Msimamizi Msaidizi wa miradi ya kijamii wa WCS akifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete (mwenye suti ya kaki waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa TAJATI na baadhi ya watumishi wa WCS na Halmashauri.

Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Kitulo akitoa maelezo kwa wanachama wa TAJATI walimpomtembelea ofisini kwake

Wanachama wa TAJATI wakiwa ndani ya Hifadhi ya Kitulo

Faraja Dembe msimamizi msaidizi wa Miradi ya kijamii kutoka WCS akionesha eneo ambalo limeondolewa mimea vamizi kupisha uoto wa asili

Ua aina ya Chikanda linalopatikana Kitulo

Mbunge wa Makete Dk. Norman Sigalla King akisalimiana na Mwanachama wa TAJATI baada ya kukutana katika Ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

Watumishi wa WCS wakiwaongoza wanachama wa TAJATI walipotembelea ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

Moja ya Maua aina 40 zinazopatikana katika hifadhi ya Kitulo pekee

Aina ya Mimea Vamizi ndani ya Hifadhi ya Kitulo ikiwa imeshaangushwa tayari kuondolewa

Wana TAJATI  wakiwa kwenye moja ya magari yaliyotolewa na WCS kwa ajili ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Kitulo




SHIRIKA la WCS lililochini ya Mpango wa Shirika la msaada la Serikali ya watu wa Marekani(USAID) mwishoni mwa wiki liliwawezesha waandishi wa habari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Kitulo.

Waandishi waliowezeshwa kutembelea hifadhi ya Kitulo ni Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji nchini Tanzania (TAJATI).

Katika ziara hiyo Wanatajati walitembelea hifadhi ya Kitulo kwa lengo la kujitambulisha ikiwa ni siku chache tangu kupata usajili na msajili wa vyama vya Kijamii chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka Mwakilili alisema lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kujitambulisha pamoja na kutembelea miradi inayoendeshwa na WCS ili kujionea changamoto na mafanikio wanayokutana nayo.

Alisema mbali na kujionea Shughuli za WCS pia walipata fursa ya kukutana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete ambaye alieleza fursa zinazoweza kupatikana ikiwa Wilaya hiyo itatangazwa vizuri.

Kwa upande wao,WCS wakiongozwa na Msimamizi msaidizi wa miradi ya kijamii, Faraja Dembe na Muikolojia Vicky Felix walisema mradi unaoendelea ni uondoaji wa mimea vamizi katika Hifadhi ya Kitulo.

Walisema mimea hiyo inachangia kuondoa uoto wa asili na kukausha vyanzo vya maji ya Mto Ruaha na ziwa Nyasa.

Waliitija aina ya mimea inayoondolewa kuwa ni pamoja na miti aina ya Cyprus, Pine, Black wattle na Eucalyptus ambayo ilipandwa kwa lengo la kupunguza ardhi oevu katika makazi ya watu kabla ya kuwa hifadhi.


No comments: