Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Taaluma, Profesa Saimon Msanjila akifungua semina ya siku mbili ya ujasiliamali kwa Wahitimu wa CBE Kampasi ya Mbeya(hawapo pichani) |
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma CBE miaka ya nyuma(ALUMNI) Boyd Mwakyusa akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wahitimu wa chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya. |
Katibu wa ALUMNI ambaye pia ni mkufunzi wa Ujasiliamali, Graciano Kunzugala, akitoa utambulisho kwa wageni na wanafunzi waliohudhuria mafunzo ya ujasiliamali |
Baadhi ya Watumishi wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Kampasi ya Mbeya wakijiandaa kupokea wageni kwa ajili ya mafunzo ya ujasiliamali katika ukumbi wa Hoteli ya Mount Livingstone |
Kunzugala akiendelea kutoa mafunzo kwa wahitimu |
Wahitimu wakifuatilia kwa makini semina inayotolewa |
WAHITIMU wa Chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE)Kampasi ya Mbeya wamepatiwa mafunzo ya ujasiliamali ili kujiandaa
na soko la ajira pindi watakaporudi uraiani.
Wahitimu hao wamepatiwa mafunzo
ya siku mbili yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mount livingstone
iliyopo jijini Mbeya mafunzo yaliyoandaliwa na Umoja wa Wanafunzi waliowahi
kusoma CBE miaka ya Nyuma Kanda ya Nyanda za juu kusini( ALUMNI).
Akizungumza katika ufunguzi wa
Semina hiyo iliyofunguliwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha CBE Taaluma, Profesa
Saimon Msanjila, Mwenyekiti wa ALUMNI Kanda ya Nyanda za juu kusini, Boyd
Mwakyusa amesema lengo la mafunzo ni kuwaandaa wahitimu kujiajiri wenyewe.
Alisema mafunzo ya siku mbili
pia yatahudhuriwa na baadhi ya watu mashuhuri ambao walisoma CBE miaka ya nyuma
na kupata mafanikio ili waweze kutoa changamoto na njia zilizowasaidia kupata
mafanikio.
Awali akifungua mafunzo hayo,
Profesa Msanjila alisema majukumu ya wahitimu ni kukisaidia Chuo kwa
kukitangaza na kufanya mambo mazuri kwenye kazi na jamii jambo ambalo
litasaidia kuleta sifa nzuri ya Chuo na hatimaye kuongeza idadi kubwa ya
wanafunzi.
Msanjila alisema Wahitimu
wanapaswa kwenda kuwa mabalozi wa Chuo kila mahali watakapokuwepo ambapo hivi
sasa Chuo kimeshinda kuwa Chuo chenye mabadiliko Chanya kwa mwaka 2015 na kuzawadiwa cheti.
“Mnapoenda huko mkafanye kazi
vizuri pia mnayonafasi ya kujiuliza namna mlivyopokelewa chuoni wakati mnaanza
pia mjitafakari namna mtakavyoendelea kutoa michango yenu kwa uongozi wa Chuo”
alisema Makamu Mkuu wa Chuo.
Kwa upande wake Katibu wa
ALUMNI, Graciano Kunzugala ambaye pia ni mkufunzi wa ujasiliamali alisema Mkioa
ya nyanda za Juu kusini inakabiliwa na tatizo la Biashara kwani asilimia kubwa
hufanya biashara ya kubangaiza na kuigana.
Alisema mfanyabiashara wa kweli
ni mjasiliamali kwani anafanya biashara yenye malengo ya muda mfupi, kati na
muda mrefu pia anakuwa na mikakati inayolenga kukuza biashara yake yenye
mwelekeo wa kukuza uchumi.
No comments:
Post a Comment