|
Washtakiwa wa uhujumu uchumi wakiwa kizimbani kutoka kulia ni Song Lei, Xiao
Shaodan, Chen Jianlin na Hu Liang. |
|
Wakili anayewatetea Washtakiwa wa Uhujumu Uchumi, Ladislaus Lwekaza akizungumza na wachina kabla ya kuanza kusikiliza kesi yao. |
|
Waendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa (kushoto) na Wankyo Saimon wakibadilishana mawazo wakisubiri kesi kuanza kusikilizwa |
|
Lwekaza akimsikiliza Mkalimani wa lugha ya kichina Manfred Lyoto alipokuwa akizungumza na wachina |
|
Maafisa wa Polisi na Forodha wakionesha Pembe za Faru ambazo walikamatwa nazo raia wa China |
|
Wachina wakipanda kwenye karandinga la Polisi tayari kurudishwa Rumande baada ya kesi yao kuahirishwa |
|
Wachina wakiingia kwenye Chumba cha Mahakama. |
RAIA wanne wa China juzi
walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya wakituhumiwa kwa makosa
matatu ikiwemo kupanga na kutekeleza njama za uingizaji wa pembe za faru nchini
bila kibali cha Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.
Washtakiwa hao walisomewa
mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Michael Mteite na mwendesha mashtaka wa
Serikali Archiles Mulisa ambaye aliwataja washtakiwa kuwa ni Song Lei, Xiao
Shaodan, Chen Jianlin na Hu Liang.
Mulisa alidai mahakamani hapo
kuwa watuhumiwa walikamatwa eneo la mpakani Kasumulu wilayani Kyela wakiwa na
vipande 11 vya pembe za Faru vyenye thamanbi ya shilingi 902,880,000 wakitoka
navyo nchini Malawi kinyume cha sheria kifungu cha 5 cha mwaka 2009 cha sheria
ya wanyama pori.
Mulisa aliyataja makosa mengine
katika kesi namba 6 ya mwaka 2015 kuwa ni kujihusisha na nyara za serikali
kinyume cha sheria za wanyamapori na kuhujumu uchumi na kosa linguine ni
kumiliki nyara za serikali bila uhalali na kinyume cha sheria ya uhifadhi ya
wanyama pori.
Washtakiwa wote walikana
mashtaka ambapo upande wa Mashtaka ulisema unao mashahidi watano na upelelezi
umekamilika na wapo tayari kuendelea na kesi huku upande wa utetezi ukitetewa
na Wakili Ladislaus Lwekaza ukiwa hauna kipingamizi.
Hakimu Mkazi Mteite aliahirisha
Kesi hadi siku inayofuata kwa ajili ya kuendelea kusikiliza mashahidi
watakaoletwa na upande wa Jamhuri.
No comments:
Post a Comment