Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Benki ya NMB Tawi la Mlowo wilayani Mbozi. |
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za juu kusini, Lucresia Makiriye akitoa taarifa ya ukarabati wa matawi ya benki hiyo wakati wa sherehe za kuzindua tawi la Mlowo |
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlowo Hemedi Risasi akitoa utambulisho katika hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akifurahia jambo na Meneja wa NMB Kanda Lucresia Makiriye alipokuwa akizindua rasmi Tawi la NMB Mlowo. |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akikata utepe kuashiria uzinduzi wa benki ya NMB Tawi la Mlowo. |
Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za juu kusini, Lucresia Makirie akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa benki ya NMB. |
Wateja wa Benki ya NMB Tawi la Mlowo wakifuatilia sherehe za uzinduzi wa tawi hilo |
Watumishi wa Benki ya NMB Tawi la Mlowo na ofisi ya kanda wakifuatilia sherehe za uzinduzi wa tawi hilo. |
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas
Kandoro ametoa wito kwa Wafanyabiashara kuacha tabia ya kuhifadhi fedha ndani
na madukani mwao na badala yake wajenge utamaduni wa kutunza benki.
Kandoro alitoa wito huo
alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Benki ya NMB Tawi la
Mlowo lililopo wilayani Mbozi Mkoa wa
Mbeya ambapo alisema tabia ya kuhifadhi fedha majumbani na madukani
inahatarisha maisha ya mfanyabiashara.
Alisema wapo wafanyabiashara
wengi ambao huvamiwa na majambazi kutokana na kutokuwa na historia ya kupeleka
fedha benki hivyo kufanya kufuatiliwa kwa ukaribu na baadaye kuporwa hivyo
kurudisha nyuma ukuaji wa uchumi.
“Zipo baadhi ya tabia za
Wafanyabiashara kuchimbia fedha ndani ya nyumba zetu na dukani eti raha yako ni
kuziona zikiongezeka lakini unasahau kuwa unahatarisha maisha kwa kuwavutia
majambazi ambao wanazitamani fedha hizo ebu kuweni na utaratibu wa kuhifadhi
kwenye mabenki” alishauri Kandoro.
Aliongeza kuwa mbali na
kuhatarisha maisha kutokana na kuhifadhi fedha mahala pasipokuwa salama pia
kuna majanga ya moto ambayo hutokea bila taarifa hivyo mfanyabiashara kushindwa
kabisa kuokoa kitu chochote zikiwemo za mtaji.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema
wafanyabiashara wakiwa na mazoea ya kutumia mabenki pia itarahisisha
upatikanaji wa mikopo mikubwa ambayo endapo watakuwa wakirejesha kwa wakati
kero ya Riba kubwa inaweza kuondolewa na hatimaye biashara na hali ya uchumi
inaweza kukua.
Awali akimkaribisha Mkuu wa
Mkoa kuzindua Tawi hilo, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Lucresia
Makiriye alisema uzinduzi na uanzishwaji wa tawi hilo umetokana na mwamko wa
wafanyabiashara kutumia benki hiyo kuhifadhi fedha pamoja na kasi ya ukuaji wa
mji wa Mlowo.
Alisema mbali na kukua kwa kasi yamaendeleo ya mji wa Mlowo pia ni
utaratibu wa Benki hiyo kuhakikisha inatanua matawi yake ili kuwafikia wateja
walipo kulingana na kauli mbiu ya Karibu yako ili wateja wengi zaidi waweze kufikiwa
na huduma.
Aliongeza kuwa pamoja na
kufungua tawi hilo pia Benki inautaratibu wa kutenga asilimia moja ya faida kwa
ajili ya shughuli za maendeleo katika jamii ambapo tayari imetoa msaada wa
madawati kwa Shule za msingi za Itete na Mlowo yenye thamani ya shilingi
Milioni 10.
No comments:
Post a Comment