Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, November 12, 2015

WAKULIMA WA TUMBAKU CHUNYA WAILILIA SERIKALI

Mkulima wa Tumbaku wilayani Chunya,Hamis Mwandura akionesha sehemu ya kukaushia zao hilo.

Hamisi akiwa akionesha jiko la kukaushia Tumbaku.

Kuni hutumika zaidi katika uandaaji wa zao la Tumbaku


SERIKALI imetakiwa kuwasaidia wakulima wa zao la Tumbaku katika kupanga bei ili kuepuka mgogoro kati ya mkulima na mnunuzi.

Wito huo ulitolewa  na Wakulima wa Tumbaku katika kata ya Mtanila wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kuhusianaa na changamoto zinazowakabili.

Wakulima hao wameiomba serikali kuingilia katika upangaji bei wa zao hilo badala ya kumwachia mkulima kupanga bei na mnunuzi pekee kwani kuna upande unaonewa.

Wakulima hao walisema kwa serikali kujiondoa kwenye usimamizi wa bei ya zao hilo kunasababisha wakulima kunyonywa kwa wanunuzi kujipangia bei zilizo na maslahi yenye kuegamia upande wao.


Akibainisha hali hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha msingi cha wakulima wa Tumbaku katika kijiji cha Igangwe, kata ya Mtanila(Igangwe Amcos) Gulila Mwakosya alisema wakulima wanaamini wananyonywa kwakuwa mara zote wanunuzi wamekuwa wakinunua kwa bei wanayoijua wao wakisema ndiyo inayoendana na soko la kimataifa.

Mwakosya alisema ni vigumu kwa mkulima kutokubaliana na bei inayopendekezwa na mnunuzi kwakuwa ni mtu wa chini asiyeweza kujua bei ya tumbaku katika soko la kimataifa.

Alisema kwa serikali kuingilia kati upangaji bei ya tumbaku itawezesha pande zote mbili kunufaika kwa usawa kwakuwa yenyewe ina uwezo mkubwa wa kutambua bei ya zao hilo katika soko la dunia.

Aliongeza kuwa endapo Serikali itapanga bei mnunuzi hata kuwa na nafasiya kujiamlia badala yake atafuata bei elekezi ambayo itaendana na ongezeko la bei ya pembejeo za kilimo pamoja na gharama za kuhudumia zao hilo.

Kwa upande wake mmoja wa wakulima wa kijiji cha Igangwe, Hamis Mwandura,  alisema serikali pia inapaswa kusimamia wanunuzi kuendeleza utaratibu wa kukutana na wakulima wa zao hilo mara kwa mara na kujadiliana kwa pamoja mambo yenye kuleta ushirikiano endelevu.

Alisema gharama za kuandaa shamba, kusia mbegu, kupandikiza na kuanza kuhudumia miche gharama yake ni kubwa lakini kipindi cha mavuno wanunuzi huja na bei zao bila kujali mkulima alitumia shilingi ngapi.No comments: