Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akizungumza katika mkutano na madereva wa magari makubwa Mpemba wilayani Momba. |
Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Shaban Mdem akitoa taarifa fupi kuhusu maendeleo ya madai ya mareva kutoka serikalini na Wamiliki. |
Naibu Katibu Mkuu na Msemaji wa Umoja wa Madereva, Rashid Saleh akizungumza katika kikao cha Madereva |
Baadhi ya madereva waliojitokeza katika mkutano uliofanyika Mpemba Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya. |
WAMILIKI wa Magari ya
usafirishaji wametakiwa kutowapangia madereva wao juu ya kumchagua mgombea Fulani
katika uchaguzi mkuu kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Aidha wamepaswa kuwaachia wao
wenyewe kumchagua kiongozi ambaye wanaona ana sera nzuri na zenye kumgusa
mhusika moja kwa moja na sio kwa shinikizo lenye kuendelea kumkandamiza dereva.
Wito huo ulitolewa na
Mlezi wa Umoja wa Madereva Tanzania(TADWU), Paul Makonda ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni alipokuwa akizungumza nao katika mkutano wao uliofanyika
katika ukumbi wa Hoteli ya Uwanji iliyopo Mpemba wilayani hapa Mkoa wa Mbeya.
Makonda alisema zipo dalili za
wamiliki wa magari kuwapangia madereva mtu wa kumpigia kura katika uchaguzi
ujao jambo ambalo linaondoa demokrasia na uhuru wa Mtanzania kumchagua kiongozi
anayemtaka na anayeona anafaa kuwaletea maendeleo.
“Zipo taarifa kuwa wamiliki
wanawashinikiza kumchagua kiongozi Fulani hili sio jambo zuri pimeni wenyewe ni
nani anagusa maslahi yenu na yupi akiingia ikulu atawasaidia moja kwa moja hao
wamiliki wanawashinikiza mmchague wanaemtaka ili waendelee kuwakandamiza hivyo
kuweni makini” alisisitiza Makonda.
Aliongeza kwa kuwahimiza
madereva hao kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kumchagua kiongozi
bora na kwamba wasimchague ambaye anatoa ahadi ya kuongeza boda boda ili hali
wao wanaendesha magari.
“Hakikisheni siku ya uchaguzi
mnajitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura ila usitake kumchagua kiongozi kwa
ahadi ya boda boda wakati wewe unaendesha Roli itakusaidiaje” alisema Mlezi
huyo.
Makonda alisema uchaguzi wa
mwaka huu ni muhimu kwa sababu umejaa historia na ni uchaguzi wa kimapinduzi
kwani inaonesha kila awamu kuwa na mabadiliko tangu awamu ya kwanza hadi awamu
ya nne hivyo awamu ya tano inapaswa kufuata mtililiko huo.
Alisema awamu ya kwanza Mwalimu
Nyerere alikuwa mkali lakini alipombadili Rais Mwinyi katika awamu ya pili
alikuwa mpole ndipo alipoingia Benjamini Mkapa katika awamu ya tatu akiwa mkali
na sasa Rais anayemalizia muda wake Jakaya Kikwete ni Mpole hivyo anapaswa
kufuatwa na Rais wa awamo ya tano ambaye ni mkali.
Awali Mwenyekiti wa Umoja wa
Madereva(TADWU), Shaban Mdem, alimpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo kwa jinsi
alivyojitoa kupigania maslahi yao na hatimaye kufikia katika hatua nzuri kati
ya Serikali, Wamiliki na Madereva.
Alisema kwa muda mfupi
wamefanikiwa kusajili Chama cha wafanyakazi ambacho katika umoja huo wameweza
kukutana na Rais ili kuzungumzia changamoto walizikuwa nazo ambazo zilizpelekea
kuwepo kwa migomo na hatimaye kufikia katika hatua nzuri.
Alisema mambo ambayo wameshakubalina
bado hatua za mwisho ni kuhusiana na posho ambapo kila dereva atapaswa kulipwa
shilingi 70,000 kwa siku kutoka Dar es salaam hadi Tunduma pamoja na fedha ya
safari shilingi 35,000 na kwamba baada ya kuvuka geti Dereva atalipwa dola 75
kwa siku.
Akizungumzia suala la wamiliki
kuwataka kumchagua kiongozi wanayemtaka wao Mwenyekiti huyo alisema jambo hilo
lipo na tayari madereva zaidi ya 40 walibainika kusambaza ujumbe mfupi wenye
kumpigia debe kiongozi wanaemtaka wamiliki.
Alisema hata hivyo madereva hao
walionywa kutoendelea na hatua hiyo na kusubiri tamko la madereva kwa pamoja
juu ya kiongozi anayepaswa kupigiwa kura tofauti na shinikizo la wamiliki.
No comments:
Post a Comment