Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, September 16, 2015

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI KIWANDA CHA TBL, WAFANYABIASHARA NCHINI WAPEWA WITO.

 Meneja wa Kiwanda cha bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliofanya ziara ya mashindano ya kuonja bia hivi karibuni(hawapo pichani)
  Meneja mawasiliano wa  TBL Makao makuu, Editha Mushi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya.
 Meneja wa Kiwanda cha bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliofanya ziara ya mashindano ya kuonja bia hivi karibuni
  Waandishi wa Mkoa wa Mbeya wakipata maelezo lutoka kwa Meneja wa kiwanda.
 Baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye chumba cha mikutano wakisubiri maelekezo.
 Mmoja wa wafanya kazi wa Tbl Mbeya akisambaza vinywaji kwa washiriki wa shindano la kuonja bia kabla ya kuanza.
 Washiriki wa mashindano wakiendelea ma zoezi
 Washiriki wa shindano la kuonja nia wakiwa makini kugundua aina ya bia iliyomo kwenye grasi.

 Mshindi wa kwanza katika shindano la kuonja bia, David Nyembe kutoka Mbeya fm akikabidhiwa zawadi na Meneja wa kiwanda cha Tbl Mbeya Waziri Jemedari.

 Mshindi wa pili katika shindano la kuonja bia, Emmanuel Lengwa kutoka ITV akikabidhiwa zawadi na Meneja wa kiwanda cha Tbl Mbeya Waziri Jemedari.
 Joseph Mwaisango akipokea grasi tayari kwa ajili ua kujaribu bahati yake.
 Baadhi ya watumishi wa TBL Mbeya wakifuatilia kwa makini shindano la waandishi la kuonja bia.
  Mkuu wa usalama wa mahali pa kazi wa TBL Mbeya, Godfrey Kisulilo akiwaonesha waandishi wa habari namna ya kutunza maji.
  Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na uomgozi wa tbl.
Waandishi wa habari Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara katika kiwanda cha bia cha TBL Mbeya.

WAFANYABIASHARA mkoani Mbeya wamehimizwa kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda cha bia cha TBL mkoani kwao kwa kujihusisha na biashara zenye mahusiano na kiwanda hicho ili waweze kunufaika na uwepo wake.
Miongoni mwa fursa zilizopo ni pamoja na kuanzisha viwanda kwaajili ya kusaga unga wa mahindi utumikao katika kutengenezea bia.
 Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya Waziri Jemedari alitoa hamasa hiyo alipozungumza na wanahabari mkoani hapa kwenye shindano la kuonja na kutambua ladha ya bia lililofanyika kiwandani na kuwashirikisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali.
Jemedari alisema bado wafannya biashara na wakulima mkoani Mbeya hawajaitumia vyema fursa ya uwepo wa kiwanda hicho hatua inayopelekea wenzao kutoka maeneo ya mbali kunufaika na fursa hiyo.
Alisema licha ya mkoa wa Mbeya kuwa miongoni mwa mikoa inayozalisha kwa wingi mahindi,bado kiwanda hicho kinalazimika kuagiza unga kutoka Arusha,Iringa,Kibaigwa na Dar es salaam.
“Wafanyabiashara wa Mbeya bado wamejikita katika biashara nyingine ikiwemo ya kununua nafaka kutoka kwa wakulima na kuziuza tena pasipo kuziongezea thamani.Hii inatulazimu kuagiza unga wa mahindi wa dona kutoka mbali wakati hapa mahindi yanalimwa kwa wingi.”
“Nadhani hawajatambua uwepo wa kiwanda hiki unavyoweza kuwanufaisha.Hatuwezi kufungua viwanda vya kusaga unga wa dona kwakuwa tutakuwa tunawanytima wengine fursa.Sisi tunatengeneza bia,tunahitaji wadau wengine wa kutuzalishia malighafi za kulisha kiwanda chetu” alisisitiza.
Alisema kwa sasa mahitaji ya unga wa mahindi wa dona kiwandani hapo ni mkubwa ambapo jumla ya tani 30 hutumika kwa kila juma moja hivyo ni fursa nzuri kwa watakaopenda kuwekeza kwenye uzalishaji wa malighafi hiyo.
Alisema TBL iko tayari kukutana na mfanyabiashara yeyote atakayeonesha nia ya kuwekeza katika biashara hiyo na itahakikisha inampa mwongozo juu ya namna gani malighafi inayohitajika na kiwanda inavyopaswa kutengenezwa.
Aliitaja fursa ya kilimo cha Shayiri kuwa faida nyingine ambayo wakazi wa Mbeya hawajawekeza ipasavyo kwani hadi sasa kwa mkoani hapa ni wakulima wa wilaya ya Mbozi pekee wanaozalisha huku kiwanda kikilazimika kununua bidhaa hiyo kutoka maeneo mengine ikiwepo Sumbawanga mkoani Rukwa.
Alisema licha yak ampuni kutoa fursa ya kuwawezesha wakulima katika shughuli mbalimbali za uzalishaji wa zao hilo,bado mwitikio wa wakulima mkoani hapa ni mdogo mno katika kilimo cha zao la Shayiri wakati soko ni la uhakika.
Katika shindano la kuonja bia,mtangazaji wa Mbeya FM David Nyembe aliibuka mshindi akifuatiwa na mwakilishi wa ITV mkoani hapa Emmanuel Lengwa aliyeshika nafasi ya pili.

No comments: