Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, September 21, 2015

MAKAMU WA RAIS MOHAMED GHARIB BILAL AHUDHURIA KUWEKWA WAKFU ASKOFU KENAN PANJA MJINI TUKUYU




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro  alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule  wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim  Panja zilizofanyika katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya.
Kwaya ya Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo kuu la kusini wakitoa burudani wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu Kenan Salim Panja iliyofanyika katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na  Askofu mteule wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim  Panja wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu iliyofanyika  katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia waumini mbali mbali katika ibada  maalum ya kuwekwa wakfu Askofu Kenan Panja.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimpongeza Askofu mteule wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim  Panja baada ya kumalizika kwa  sherehe ya kuwekwa wakfu iliyofanyika  katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya.

Picha na OMR.


No comments: