Mtia nia wa udiwani Kata ya Ndanto Wilaya ya Rungwe, Award
Mpandila akikabidhiwa fomu ya kugombea udiwani na Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo,
Emmanuel Kajuni.
|
.Mtia nia ya Udiwani Award Mpandila akizungumza na
wanahabari pamoja na wananchi lukuki waliojitokeza kumsikiliza.
|
Award Mtandila akisalimiana na baadhi ya wananchi
waliojitokeza kumsikiliza.
|
Wananchi wa Kata ya Ntando wakimsikiliza mtia nia ya Udiwani
Award Mtandila.
|
. Mtia nia Mtandila akiburudika pamoja na wapiga kura wake.
|
Wananchi na wanachama wa CCM wakicheza wakati wakimsikiliza
mtia nia.
|
Baadhi ya Wananchi walilazimika kuchungulia kwa mbali
kumshuhudia mtia nia alipokuwa akitoa vipaumbele vyake.
|
Msafara wa mtia nia ya udiwani ulipokua ukielekea kuchukua
fomu pamoja na kuelekea eneo la mkutanokuzungumza na waandishi wa habari.
|
KADA wa Chama cha Mapinduzi, Award Mpandila amejitokeza
kuomba ridhaa ya kuomba kuteuliwa kugombea Udiwani katika Kata ya Ndanto na
kwamba akiteuliwa atahakikisha viwanda vya kusindika mazao vinajengwa.
Alisema licha ya Wilaya ya Rungwe kuwa kitovu cha uzalishaji
wa mazao mbali mbali nchini lakini bado inakumbwa na changamoto ya ukosefu wa
viwanda vya kuongezea thamani mazao yao.
Mpandila alibainisha hayo alipozungumza na wanahabari mara
baada ya kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea udiwani
katika kata ya Ndanto wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Mpandila alisema wakazi wakata hiyo na wilaya ya
Rungwe kwa ujumla si watu wa kusukumwa katika kufanya kazi bali hujituma kwa
moyo wa dhati lakini hawajanufaika najitihada zao.
Alisema kikwazo kikubwa kwa wakazi hao ni mazao
wanayozalisha kuuzwa pasipo kuongezewa thamani hatua inayosababisha wachuuzi
kunufaika zaidi pale wanaponunua na kwenda kuuza kwenye miji mikubwa.
Alitaja zao la viazi mviringo kuwa moja ya mazao ambayo
iwapo yangeongezewa thamani kabla ya kusafirishwa yangewezesha wakulima kupata
faida kubwa na kukuza uchumi wao.
Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo,halmashauri ya
wilaya yaRungwe inahitaji kupata madiwani walio na mtazamo wa kushawishi
wawekezaji kuja kuwekeza kwa kufungua viwanda vya kusindika mazao.
Mpandila alisema ili kufanikisha hilo ameamua kujitosa
kuwania nafasi ya kuingia kwenye chombo cha maamuzi cha halmashauri na iwapo
chama kitampa ridhaa ya kugombea na hatimaye wananchi wa kata hiyo kumchagua
hilo litakuwa na kipaumbele kikubwa kwake.
Aliongeza Wilaya haiwezi kupiga hatua iwapo wananchi
wataendelea kuuza mazao yao kwa mfumo walioanza nao mababu zao hivyo lazima
waingie kwenye ukurasa mpya na wa kisasa katika uuzaji wa mazao tunayozalisha.
Alisema iwapo atapewa ridhaa atahitaji kushirikiana na wadau
kuona tunatoka hapa tulipo sambamba na utekelezaji wa masuala yatakayokuwa
kwenye ilani ya chama cha Mapinduzi.
Akizungumzia changamoto ya barabara za vijijini,Mpandila
alisema bado wakulima wanapata shida kusafirisha mazao kutoka mashambani
kuyaleta barabara kuu.
Alisema wakulima hususani katika kata ya Ndanto wanahitaji
barabara zinazopitika kwa kipindi cha mwaka mzima kwakuwa misimu ya kilimo kwao
haina ukomo.
No comments:
Post a Comment