SAKATA la unyanyasaji aliofanyiwa
mwanamke mjamzito Judith Komba siku ya kujifungua katika hospitali ya Rufaa
kitengo cha wazazi cha Meta limechukua sura mpya baada ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya
Abbas Kandoro kuagiza wauguzi waliokuwa zamu siku ya tukio wachukuliwe hatua
stahiki.
Mnamo usiku wa Mei 13 mwaka huu
mwanamke Judith Komba mkazi wa Iwambi jijini Mbeya alijikuta analazimika
kujifungulia katika kitanda cha kubebea wagonjwa ndani ya hospitali ya Meta
pasipo usaidizi wa mtu yeyote na mtoto kunusurika kifo kutokana na mazingira
hatari yaliyoukabili uzazi wake.
Hivi karibuni Judith alikaririwa na
vyombo vya habari akibainisha kuwa alilazimika kujifungulia kwenye mazingira
hayo baada ya kuwafuata mara kadhaa wauguzi waliokuwa akiwaomba wamsaidie
lakini walimpuuza na wakaendelea kulala kwenye chumba chao.
Mwanamke baada ya kuzidiwa na
kujikuta hawezi kurejea wodini alikokuwa amelazwa alijikuta analazimika kulala
kwenye kitanda cha kubebea wagonjwa akiwa amezidiwa na uchungu na akajifungulia
hapo.
Hatua hiyo imeonesha kusononesha
wadau wengi akiwemo mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye amemuagiza katibu tawal mkoa kufuatilia
suala hilo na kuwachukulia hatua stahili wauguzi waliokuwa zamu.
Kandoro alitoa agizo hilo kwenye
hafla fupi ya uzinduzi wa mpango wa miaka minne wa Kusaidia maisha ya Akina
mama wajawazito na Watoto kwa halmashauri 10 za mkoani Mbeya unaofadhiliwa na
shirika la Korea International Cooperation Agency(KOICA) kupitia Unicef.
Kandoro alisema yapo majibu
rahisirahisi yaliyotolewa na utawala wa hospitali hiyo lakini ukweli ni kuwa
majibu hayo hayatoshelezi hata kidogo ikilinganishwa na uzembe uliotokea siku
hiyo.
“Majibu yametolewa kirahisi
rahisi.Mimi nasema siyakubali na naagiza katibu tawala uhakikishe unafuatilia
jambo hilo na waliohusika wawajibishwe.Kwani hawafahamiki waliokuwa zamu siku
hiyo?Kwa nini utawala utumie lugha rahisi rahisi”
“Hatuwezi kuruhusu mtu atoe matatizo
yake nyumbani kwake ayalete kazini na kuwaumiza wasio husika na matatizo
hayo.Tumeambiwa hapa moja ya vitu vinavyochangia vifo vya wajawazito na watoto
wachanga ni uzembe wa watoa huduma.Hili lazima tulifanyie kazi haraka” alisema
Kandoro.
Chanzo Lyamba Lya Mfipa |
Thursday, June 4, 2015
KAULI YA RC KANDORO JUU YA MJAMZITO ALIYENYANYASWA HOSPITALI YA META JIJINI MBEYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment