Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, June 19, 2015

HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA YA NYANDA ZA JUU KUSINI- MBEYA, YAZINDUA MNARA WA UPASUAJI WA TUNDU DOGO(LAPARASCOPIC TOWER)

Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali kutoka Makao makuu, Dk. Magreth Mhando akikata utepe  kuzindua mnara wa upasuji wa tundu dogo (LAPARASCOPIC TOWER)

Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali kutoka Makao makuu, Dk. Magreth Mhando akiongea na watumishi na wageni waalikwa mara baada ya kuzindua mnara wa upauaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya

Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini, Dk.Mpoki Ulisubisya, akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi

Fedric Ogumbo  mkurugenzi wa kampuni ya Baylem kutoka Kenya ambaye ametoa msaada wa vifaa vya upasuaji vyenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 5000.


Baadhi ya Madkatari na wauguzi wakimsikiliza mgeni rasmi kwa makini


Dr. Lazaro Mboma mkuu wa idara ya upasuaji na Daktari bingwa upasuaji  akimwelezea mgeni rasmi jinsi mnara wa upasuaji unavyofanya kazi


Moja ya aliyetengeneza mtambo wenyewe wa upasuaji kwa njia ya tundu dogo kutoka Kampuni ya Gimmi ya Tutlingen nchini Ujerumani mkono wa kulia akielezea jinsi mtambo huo unavyofanya kazi


  MNARA WA UPASUAJI WA TUNDU DOGO(LAPARASCOPIC TOWER)


 
  HOSPITALI  ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya, imezindua mnara wa upasuaji wa tundu dogo(LAPARASCOPIC TOWER) utakaopunguza wagonjwa kuomba Rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali zingine.Akizungumza katika uzinduzi huo , Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini, Dk.Mpoki Ulisubisya, alisema msaada huo utapuguza idadi ya wagonjwa ambao wamekuwa wakiomba rufaa pia hitaji halisi la Hospitali hiyo la ufinyu wa nafasi ya kulaza wagonjwa na kupunguza msongamano wa wagonjwa.Alisema kutokana na changamoto hizo uongozi wa Hospitali ulifikiria namna ya kusogeza huduma ya upasuaji kwa njia ya Tundu dogo kwa Wagojwa ambapo ulishirikiana na wadau mbali mbali ili kufanikisha hilo na baadhi yao kuitikia na hatimaye kukubali kulitekeleza.Aliwataja baadhi ya marafiki walioitikia wito huo na kuliwezesha suala hilo kufanikiwa kuwa ni pamoja na John Fedric Ogumbo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Baylem kutoka Kenya ambaye alitoa msaada wa vifaa vya upasuaji vyenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 5000.Aliongeza kuwa Kampuni hiyo pia imesaidia Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kufadhili mafunzo kwa madaktari wanne nchini Ureno kwa gharama isiyopungua Euro 24000 hali iliyochangia Hospitali hiyo kuwa na watalaamu waliobobea kuliko Hospitali zingine nchini.Mkurugenzi huyo alisema mtu mwingine wa kumshukuru ni aliyetengeneza mtambo wenyewe wa upasuaji kwa njia ya tundu dogo kutoka Kampuni ya Gimmi ya Tutlingen nchini Ujerumani  ambao wameahidi kuhakikisha madaktari waliosomea watafanyakazi kwa weledi na ufanisi.Alizitaja kazi za mtambo huo kuwa ni pamoja na upasuaji wa mawe kwenye njia ya nyongo, upasuaji wa kidole tumbo, upasuaji wa Tezi dume na upasuaji wa magonjwa ya akina mama.Alisema faida ya mtambo huo ni pamoja na upasuaji kufanyika kwa muda mfupi tofauti na uliozoeleka, ufupi wa mgonjwa kukaa hospitalini, maumivu kidogoukilingianishwa na upasuaji mkubwa kwa njia ya visu na kuzuia damu nyingi kupotea wakati wa zoezi la upasuaji.Kwa upande wake Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali kutoka Makao makuu, Dk. Magreth Mhando alisema Wizara ya afya kupitia Sera ya Afya na mpango wa maendeleo ya afya ya msingi, sekta ya msingi na zinginezo inakusudia kuboresha mazingira ya sekta hiyo.Alisema Serikali inaipongeza Hospitali hiyo kwa juhudi ambazo inaendelea kuzifanya ambazo ni  kuwa na majengo mazuri, stahiki za watumishi, vitendea kazi, utawala bora na kumjali mteja jambo ambalo linaifanya Hospitali hiyo kuzidi kuwa bora na kuwa mfano wa kuigwa.Aidha alitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiinginza Sekta ya afya katika matokeo makubwa sasa(BRN)unaoanza kutkelezwa katika awamu ya pili ukijikita katika sehemu nne.Mwisho.
Na Mbeya yetu


No comments: