Mwili wa marehemu askari polisi a namba G 2526 DC Willium Juma aliyeuwawa na majambazi June 10 mwaka huu ukiwasili nyumbani kwake ghana kwa ajili kuagwa. |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kifo cha askari huyo. |
Ndugu na jamaa wakiomboleza msiba huo nyumbani kwake ghana leo June 11 |
Mwili wa marehemu ukitolewa ndani tayari kwa kuagwa na ndugu na jamaa |
Mke wa marehemu akifarijiwa |
Marehemu DC Willium Juma enzi za uhai wake |
Mkuu wa wilaya ya mbeya Nyiremba Munasa akitoa salamu katika msiba huo. |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akizungumza katika msiba huo |
.
ASKARI polisi namba
G 2526 DC Willium Juma, ameuawa kwa kupigwa risasi ya kifua na watu
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Marehemu, Juma inasemekana alikutwa na mauti hayo akiwa
njiani akikimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza wakati
akiaga mwili marehemu , Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed
Msangi alisema marehemu Juma alipatwa na mauti hayo akiwa njiani akikimbizwa
hospitali baada ya kupigwa risasi ya kifua na watu wanaosadikiwa ni majambazi.
Amesema, marehemu Juma pamoja na wenzake, wakiwa katika
doria ya mchana walipata taarifa ya
wahalifu hao ambao inasemekana walikuwa
katika harakati za kuwavamia raia wa kihindi wamiliki wa Kampuni ya Export
iliyopo katika eneo la Iwambi jijini Mbeya.
Alisema, inasemekana wahindi hao walikuwa wametokea
Benki kuhifadhi fedha zao hivyo
majambazi walihisi kwamba wahindi hao
walikuwa wametoka kuchukua fedha hivyo
kutaka kuwapora kwa kutumia silaha.
Kamanda Msangi, amefafanua kuwa, wakati askari wakiwa wanaangali mbinu za
kuingia kwenye eneo ilipotokea milio ya risasi, walishangaa kuona pikipiki
mbili zikiwa zimepakia watu zikija kwenye eneo lao .
Alisema, inasemekana pikipiki moja iliwapita askari hao
nay a pili ilisogea na ndipo jambazi mmoja alitoa silaha yake na kumimina
risasi hovyo ndipo moja ilimpata marehemu Willium katika kifua chake na
kumsababishia mauti yake.
Amesema, jambazi
huyo alipopigwa risasi ya mguu alifanikiwa kukimbia lakini alishindwa kuendelea
na safari yake kutokana na kupoteza damu nyingi hivyo askari kufanikiwa
kumkamata na alipoulizwa jina lake alijitambulisha kuwa anaitwa peter na kukata
roho hapo hapo.
Aidha, Kamanda Msangi, amesema jeshi la polisi
limefanikiwa kukamata silaha moja iliyotengenezwa kwa kienyeji ikiwa na risasi mbili zinazotumika kwenye
bunduki aina ya Shot gun na kwamba msako
unaendelea kwa ajili ya kuwakamata waliofanikiwa kukimbia pamoja na silaha
moja.
Hata hivyo alisema kuwa mwili wa Marehemu Willium juma, unasafirishwa
leo kwenda nyumbani kwao Mkoani Mara kwa ajili ya maziko, huku mwili wa jambazi ukiwa umehifadhiwa katika hospitali
ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
Mwisho.
Kwa hisani ya Jamii moja blog
Kwa hisani ya Jamii moja blog
No comments:
Post a Comment