KAMPUNI ya bia Tanzania (TBL) imetenga zaidi ya shilingi Milion 220 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiliamali wadogo wadogo ili kuinua mitaji yao ya biashara katika shindano la Safari lager wezeshwa.
Hayo yalibainishwa na Meneja wa Wilaya ya Mbeya wa TBL, Vivianus Lwezaura, alipokuwa akifunga mafunzo ya washindi wa Safari lager wezeshwa awamu ya nne 2014/2015 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Peter Safari iliyopo Ilomba Jijini Mbeya.
Lwezaura alisema kampuni hiyo imekuwa na utaratibu wa kutenga sehemu ya faida yake kwa ajili ya kuwainua wafanyabiashara wadogo kwa kuwapa mitaji kupitia shindano la Safari lager wezeshwa.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo, meneja huyo aliwataka washindi wa Safari lager wezeshwa kuwa mabalozi wa kampuni ya TBL waendako ili kuwahamasisha wajasiliamali wengine kujitokeza katika shindano hilo klwa kuwa ni mkombozi wa mtanzania mwenye kipato cha chini.
Alisema shindano linakuwa halina maana kama kampuni inatumia gharama kubwa kutangaza lakini wafanyabiashara wanaojitokeza wanakuwa wachache hivyo kuigharimu kampuni ambayo inatumia fedha nyingi kuwataarifu washiriki kupitia matangazo mbali mbali.
Awali akimkaribisha Meneja huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi, Mkufunzi wa Mafunzo hayo Deodati Bernard, kutoka kampuni ya Huduma ya maendeleo ya biashara(TAPBDS), alisema mchakato wa kuwapata washindi ni mgumu na hakuna upendeleo wowote unaofanyika.
Alisema katika shindano la awamu hii jumla ya Wafanyabiashara 3500 walijitokeza Nchi nzima ambapo Kanda ya Nyanda za juu kusini walikua zaidi ya 1000 lakini baada ya kupitia vigezo na masharti wakachujwa na kubaki 29 ambao walitembelewa bila wao kujijua na hatimaye kupatikana 12.
Aliongeza kuwa hao 12 baada ya kufuzu hatua zote wamepatiwa mafunzo namna ya kuendesha biashara zao kwa faida kabla ya kukabidhiwa vifaa walivyoomba kutoka katika shindano la Safari lager Wezeshwa.
Kwa upande wao washiriki walisema watakuwa mabalozi wazuri kwa wananchi ili kuwahamasisha na wao kushiriki katika mashindano yajayo ambapo washiriki hao walipata fursa pia ya kutembelea kiwanda cha bia cha TBL Mbeya kujionea shughuli zinazofanywa.
Meneja wa Wilaya(District Manager)wa TBL Mbeya, Vivianus Lwezaura akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Washindi wa safari lager wezeshwa kanda ya Mbeya.
Meneja wa Wilaya(District Manager)wa TBL Mbeya, Vivianus Lwezaura akizungumza na washiriki wakati akifunga mafunzo ya Washindi wa safari lager wezeshwa kanda ya Mbeya.
Mkufunzi wa washiriki wa safari lager wezeshwa, Deodati Bernard akimkaribisha mgeni rasmi kufunga mafunzo ya safari lager wezeshwa.
Mkufunzi mwezeshaji, Sizya Puya, akizungumza jambo katika hafla ya kufunga mafunzo ya washindi wa safari lager wezeshwa.
Meneja wa Wilaya(District Manager)wa TBL Mbeya, Vivianus Lwezaura akikabidhi vyeti kwa washiriki wa safari lager wezeshwa kanda ya Mbeya.
Moja ya Cheti walichokabidhiwa washiriki wa mafunzo ya safari lager wezeshwa.
Washiri, Mgeni rasmi na wakufunzi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vyeti vya ushiriki wa mafunzo.
Meneja wa Kiwanda cha Bia (TBL) Mbeya Waziri Jemedari akizungumza na washindi wa safari lager wezeshwa baada ya kutembelea kiwanda hicho.
Meneja wa usalama mahala pa kazi katika kiwanda cha Bia Mbeya, Godfrey Kisulilo, akitoa maelekezo kwa washindi wa safari lager wezeshwa mara baada ya kutembelea kiwanda hicho.
Mkuu wa Matukio wa TBL Kanda ya Mbeya, Abubakari Masoli akiwasikiliza washindi wa safari lager wezeshwa baada ya kutembelea kiwanda.
Washindi wakifuatilia kwa makini maelezo wanayopatiwa
Mwanafunzi wa ufundi, Heri Mwainyekule akitoa maelekezo kwa washindi wa safari lager wezeshwa baada ya kutembelea kiwanda.
Washindi wa safari lager wezeshwa wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuzungukia kiwandani.
Washindi wa safari lager wezeshwa wakiwa ndani ya kiwanda cha bia Mbeya wakijifunza mambo mbali mbali ya uzalishaji.
Washindi wakifurahia baadhi ya vinywaji vinavyozalishwa na kiwanda cha bia cha Mbeya.
Picha na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment