WATUMISHI
wanawake wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Mkoa wa Mbeya wametembelea
Hospitali ya Wazazi Meta na kutoa misaada mbali mbali ikiwa ni kusherekea siku
ya wanawake duniani.
Akizungumza
baada ya kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Watumishi wenzake, Tuli Mwakyusa,
alisema wameguswa na kitendo cha wanawake wenzao kuwa Hospitali na kushindwa
kufanya kazi zinazoweza kuwaingizia kipato.
Mwakyusa
alisema ili kuadhimisha siku ya Wanawake duniani wameona wakatumia nafasi hiyo
kuwafariji wanawake wenzao waliolazwa Hospitalini kutokana na shida mbali mbali
sambamba na wengine kujifungua watoto katika siku hiyo.
Mtumishi
mwingine wa NHIF, Anatolia Lusasi, alisema si rahisi sana kujua mahitaji ya
wanawake waliopo Mahosipatilini pasipo kuwatembelea na kujua shida zao.
“
Tukiwa tunatembea barabarani hatujui wenzetu waliolazwa wanashida gani lakini
sisi leo tumekuja tumejionea jinsi hali halisi ilivyo na ndiyo maana tukaona ni
vema tukatoa chochote” alisema Lusasi.
Aliongeza
kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa jamii kujenga utamaduni wa kuwatembelea mara kwa
mara wagonjwa walioko Hospitalini kwani ni wengi ambao wanakosa msaada kutokana
na kutokuwa na ndugu na jamaa wakuweza kuwapa huduma.
Alisema
wakiwa hospitali hapo wamejifunza mambo mbali mbali zikiwemo huduma zitolewazo
na Hospitali ya Wazazi Meta hususani kuwahudumia akina mama wanaojifungua
pamoja na utunzaji wa watoto wachanga waliozaliwa kabla ya muda kufika.
Aidha
aliupongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa jitihada zake za kudumisha usafi wa
mazingira pamoja na mawodi ya wagonjwa kuwa masafi na katika mpangilio mzuri
jambo alilosema linasaidia mgonjwa kupona haraka kutokana na hali ya usafi.
Alivitaja
vitu vilivyopelekwa kuwa ni pamoja na Sabuni za mche Katoni 5, sabuni za
unga boksi 3,Pedi katoni 3 na Nepi dazani 3 vyote vikiwa na thamani ya
shilingi Laki moja na nusu.
Alisema
mchango huo umetolewa na watumishi wanawake wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa
Mbeya wakiwa sita walioongozana pamoja kuwatembelea wagonjwa hospitalini hapo
ambao ni Anatolia Lusasi, Tuli Mwakyusa, Emma Mdoe, Egdia Kyabona, Pendoeva
Kapola na Esther Haule.
Akishukuru
kwa ajili ya Msaada huo, Muuguzi wa Zamu wa Hospitali ya Wazazi Meta, Salome
Mpogole, aliwapongeza watumishi wa NHIF kwa moyo waliounesha kwa kuwatembelea
wagonjwa na kutoa msaada huo.
Alisema
katika usiku wa kuamkia Machi 8, mwaka huu ambayo ni siku ya Wanawakle duniani
katika Hospitali hiyo wamezaliwa watoto sita ambao wote ni wa kike.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment