Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, March 18, 2015

RUFAA MBEYA ANAKOENDELEA NA MATIBABU BARAKA COSMAS ATEMBELEWA NA NAIBU WAZIRI WA AFYA, DK. STEVEN KEBWE HOSPITALINI.

Naibu Waziri wa Afya na ustawi wa jamii, Dk. Steven Kebwe akifurahia baada ya kukuta hali ya mtoto Baraka Cosmas(6) aliyelazwa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya baada ya kukatwa kiganja na watu wasiojulikana.

Naibu Waziri wa Afya na ustawi wa jamii, Dk. Steven Kebwe akiwa na  mtoto Baraka Cosmas(6) aliyelazwa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya baada ya kukatwa kiganja na watu wasiojulikana alipofika kumjulia hali.

Naibu Waziri wa Afya na ustawi wa jamii, Dk. Steven Kebwe akimpa pole  mtoto Baraka Cosmas(6) aliyelazwa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya baada ya kukatwa kiganja na watu wasiojulikana.

Naibu Waziri wa Afya na ustawi wa jamii, Dk. Steven Kebwe akiwa sambamba na muuguzi Mkuu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya wakimjulia hali mtoto Baraka Cosmas(6) aliyelazwa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya baada ya kukatwa kiganja na watu wasiojulikana.

Naibu Waziri wa Afya na ustawi wa jamii, Dk. Steven Kebwe pamoja na uongozi aliofuatana nao kutoka Wizarani wakimjulia hali  mtoto Baraka Cosmas(6) aliyelazwa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya baada ya kukatwa kiganja na watu wasiojulikana.




NAIBU waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Steven Kebwe amemtembelea mtoto Baraka Cosmas(6) mwenye ulemavu wa ngozi(albino) aliyelazwa katika hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya baada ya kukatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiofahamika.

Akiwa katika Wodi ya Watoto alikolazwa mtoto huyo, Dk. Kebwe alisema ni vizuri akaanza shule mara baada ya kupona jeraha lake ili aweze kuzoea kutumia mkono wa kushoto baada ya mkono wa kulia kuondolewa kiganja ambapo hivi sasa hali yake inaendelea vizuri.

Naibu waziri huyo alisema kwa umri alionao Baraka alipaswa kuanza shule hivyo akasisitiza kuwa ni muhimu mara tu baada ya kupona jeraha lake akapelekwa shule akiwa katika mazingira yatakayoandaliwa kiusalama kwake na kwa walemavu wengine wa ngozi.

Alisema kukosa kiganja cha kulia si sababu ya mtoto huyo kukosa elimu kwakuwa kutokana na umri wake mdogo bado anaweza kusaidiwa kuanza kutumia mkono wake wa kushoto katika shughuli mbalimbali ikiwemo masomo.
  
Aidha naibu waziri huyo alisisitiza waganga wa jadi wanaopotosha  umma kuendelea kufichuliwa na jamii huku pia akizitaka halmashauri zilizochelewa kuondoa mabango ya waganga wa jadi kufanya hivyo haraka.

Dk.Kebwe alisema suala la mapambano dhidi ya ukatili unaofanywa kwa watu wenye ualbino ni la kila mwana jamii hivyo hakuna mtu anayepaswa kulifumbia macho badala ya kutoa ushirikiano wa dhati.

Alisema serikali bado inaendelea na mikakati madhubuti itakayowaweka watu wenye ulemavu huo kwenye mazingira salama sambamba na kuwawajibisha watu wote watakaobainika kuhusika na vitendendo vya ukataji wa viungo ama mauaji ya watu hao.

Mwisho.
Na Mbeya yetu
   

No comments: